Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) Profesa George Msalya akizungumza jambo wakati akitoa mada katika warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika leo Mei 21 , 20224 katika ukumbi wa mikutano wa TVLA jijini Dar es Salaam , warsha hiyo imelenga kuwajengea uwelewa wanahabari kuhusu tasnia ya maziwa kuelekea Maadhimisho ya wiki ya Maziwa kwa mwaka huu yanatarajia kufanyika Mkoani Mwanza ambapo yamebeba kauli mbiu isemayo : Kunywa Maziwa Salama kwa Afya Bora na Uchumi Endelevu.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) Profesa George Msalya akikabidhi Maziwa kwa waandishi wa habari walioshiriki warsha iliyofanyika leo Mei 21 , 20224 katika ukumbi wa mikutano wa TVLA jijini Dar es Salaam , warsha hiyo imelenga kuwajengea uwelewa wanahabari kuhusu tasnia ya maziwa kuelekea Maadhimisho ya wiki ya Maziwa kwa mwaka huu yanatarajia kufanyika Mkoani Mwanza ambapo yamebeba kauli mbiu isemayo : Kunywa Maziwa Salama kwa Afya Bora na Uchumi Endelevu.
Watoa mada wakizungumza jambo katika warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika leo Mei 21 , 20224 katika ukumbi wa mikutano wa TVLA jijini Dar es Salaam , warsha hiyo imelenga kuwajengea uwelewa wanahabari kuhusu tasnia ya maziwa kuelekea Maadhimisho ya wiki ya Maziwa kwa mwaka huu yanatarajia kufanyika Mkoani Mwanza ambapo yamebeba kauli mbiu isemayo : Kunywa Maziwa Salama kwa Afya Bora na Uchumi Endelevu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika warsha iliyofanyika leo Mei 21 , 20224 katika ukumbi wa mikutano wa TVLA jijini Dar es Salaam , warsha hiyo imelenga kuwajengea uwelewa wanahabari kuhusu tasnia ya maziwa kuelekea Maadhimisho ya wiki ya Maziwa kwa mwaka huu yanatarajia kufanyika Mkoani Mwanza ambapo yamebeba kauli mbiu isemayo : Kunywa Maziwa Salama kwa Afya Bora na Uchumi Endelevu.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) Profesa George Msalya amewataka wadau mbalimbali nchini kuchangamkia fursa ya kufanya uwekezaji katika sekta ya maziwa kwani uzalishaji ni mdogo ukilinganisha na uhitaji.
Akizungumza leo Mei 21, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha kwa waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa TVLA ambayo imelenga kuwajengea uwelewa kuhusu tasnia ya sekta ya maziwa, Profesa Msalya, amesema kuwa hali ya uzalishaji wa maziwa nchini ni lita bilioni 3.9, huku uhitaji ukiwa lita bilioni 12 kwa mwaka.
Profesa Msalya amesema kwa bado kuna uhitaji wa maziwa lita bilioni 9 jambo ambalo limepelekea Serikali kuanza kuagiza maziwa ya kutoka nje ya nchi.
“Licha ya kuwa na ng’ombe wengi nchini Tanzania na kuwa wa pili katika bara la Afrika, lakini bado tunazalisha maziwa kidogo na hali hii kutokana wafugaji wengi hawatumii ng’ombe wa kisasa wa maziwa” amsema Profesa Msalya.
Profesa Msalya amesema kuwa mwaka 2023 wameagiza maziwa lita milioni 11 kutoka nchi ya zaidi ya 10 duniani ambapo watumia shilingi bilioni 23.
Amesema kuwa wakati umefika wa kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya maziwa kwa kuanza kufuga ng’ombe wa kisasa ili kuleta tija kwa Taifa.
Profesa Msalya amewakumbusha waandishi wa habari kutumi vizuri kalamu zao pamoja na kuyafanyia kazi kwa vitendo yale waliojifuza kwa ajili ya kulisaidia taifa kufahamu zaidi kuhusu tasnia ya maziwa na umuhimu wake.
Amesema kuwa bado wananchi hawana uwelewa mkubwa kuhusu unywaji wa maziwa kwani baadhi ya watu bado wanaamini maziwa kwa ajili ya watoto wadogo.
“Waandishi wa habari ni kalamu zetu ambazo tunazipeleka kwa jamii kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu umuhimu wa unywaji wa maziwa na namna bora ya kuyatunza kabla ya kumfikia mlaji” Profesa Msalya.
Profesa Msalya amesema kuwa maziwa bora yaliopo nchni ni asilimia 12 ambayo yanaingia katika mfumo rasmi kwa kuyapeleka katika vituo vya kukusanyia maziwa ambavyo vipo 252.
“Maziwa salama ni yale ambavyo yamekusanywa katika vituo vyetu 252 na kwenda viwandani kwa ajili ya kuchakatwa na kupewa namba maalamu na kuyanuza” amesema Profesa Msalya.
Ameeleza kuwa ili kuhakikisha wanafikia malengo serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wamekuwa na utaratibu wa kutoa mikopo kwa ajili ya kuwakopesha watu, taasisi kwa ajili ya kuvisaidia viwanda kuimarika pamoja na mifumo ya kukusanya maziwa
Profesa Msalya ameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na kufanya uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa maziwa.
Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi (WMU) inayosimamia Tasnia ya Maziwa ikiwa na majukumu ya kuratibu na kuhakikisha sekta ya maziwa inakuwa na tija na yenye mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi na wote wanaojihusisha na shughuli mbalimbali katika mnyororo wa thamani.
Kila mwaka tangu mwaka 1998 WMU, TDB na washirika wake wanafanya maadhimisho ya unywaji maziwa kwa kuonesha shughuli za uwekezaji na ujasiriamali katika Tasnia ili kuwavutia watu wengi wapende shughuli za Tasnia lakini zaidi kupenda kutumia maziwa na bidhaa zake.
Kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kuhabarisha umma TDB kwa kushirikiana na wadau wake imeandaa semina hiyo ili kujenga uelewa wa pamoja kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza kuanzia Mei 28, 2024 mpaka Juni 01, 2024.