Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mtandao wa Kijamii Fullshangwe, John Bukuku akiwasilisha Mada katika Kongamano la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii iliyofanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa.Kogamano hilo limefanyika leo Mei 21,2024 Jijini Dar es Salaam.
…………………
MKURUGENZI wa Mtandao wa Kijamii Fullshangwe blog, John Bukuku amesema wanahabari wa mitandao ya kijamii wanatakiwa kutambua na kuzingatia miiko na sheria zinazoongoza katika utekelezaji wa majukumu kwa lengo la kuhakikisha kuna uwepo wa utoaji wa taarifa sahihi.
Ameyasema hayo leo Mei 21,2024 wakati akiwasilisha mada katika Kongamano la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii iliyofanyika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa.
Bukuku amesema matumizi ya mitandao ya kijamii ni fursa kama itatumika vizuri hususan katika kusaidia jamii kutatua changamoto mbalimbali zinazotukabili.
Kongamano hilo limehudhuliwa na wadau mbalimbali zaidi 500 kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.