Mwakilishi wa viti maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mwanajuma Kassim Makame (kushoto) akimkabidhi simu ya kisasa (smartphone) Katibu UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja Zuwena Suleiman Ali ili kurahisisha usajili wa wanachama kieletroniki, huko Mahonda katika Ofisi za CCM Mkoa huo.
……..
Na Takdir Ali. Maelezo.
Mwakilishi wa viti maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Mwanajuma Kasim Makame amekabidhi simu za kisasa (smart phone) kwa watendaji wa UWT mkoa wa kaskazini unguja ili kurahisisha zoezi la usajili wa wanachama kielektroniki.
Ameyasema hayo huko Mahonda wakati alipokuwa akikabidihi simu hizo pamoja na kuwakabidhi kadi wanacha wapya wa UWT katika Mkoa huo.
Amesema hatua hiyo ni miongoni mwa kuunga mkono juhudi za chama cha mapinduzi katika kuongeza idadi ya wanachama hai.
Amesema kusajiliwa kwa wanachama kupitia mfumo huo,utawezesha kujuwa idadi halisi ya wanachama na kukiingizia chama mapato.
Aidha amewataka kushiriki katika vikao na kulipia ada ya kadi hizo kwa wakati ili UWT iweze kujiendesha na kufikia malengo yaliokusudiwa.
Kwa upande wao Ahmada Shaa Vuai katibu Mwenezi wa ccm katika mkao wa kaskazini Unguja na Zuwena suleiman Ali katibu wa UWT Mkoa huo, wamesema simu hizo zitakuwa chachu ya kuingiza wanachama wapya katika mfumo wa kielektronik kutoka asilimia 75 hadi kufikia 85 ifikapo januari 2025.
Nao viongozi waliokabidhiwa simu hizo wameahidi kuzitumia ipasavyo ili maelengo yaliokusudiwa yaweze kufikiwa.
Aidha wametoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano wa kiongozi huyo katika kubuni mikakati itakayokiwezesha chama hicho kupata ushindi ifikapo mwaka 2025.
Jumla ya smu tatu, zenye thamani ya zaidi ya sh. laki 7 zimekabidhiwa kwa viongozi hao sambamba na wanachama wapya 50 wa UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja kukabidhiwa kadi.