Chama kikuu cha ushirika RUNALI kimewapa Tuzo viongozi mbalimbali kwa kutambua mchango wao katika sekta ya kilimo na kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale.
Akizungumza mara baada ya Uchaguzi, mwenyekiti wa RUNALI Odas Mpunga alisema kuwa wamempa Tuzo Rais Dr Samia suluhu Hassan, waziri mkuu Kasimu Majaliwa, waziri wa kilimo Husein Bashe na mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack kwa mchango wao katika sekta ya kilimo.
Mpunga alisema kuwa kilimo kimekuwa mkombozi kwa wananchi wa wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale kutokana na serikali kuwekeza katika sekta hiyo ambayo imekuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr Samia suluhu Hassan imekuwa msaada mkubwa katika kukuza uchumi kwa wakulima hasa pale ambapo serikali imekuwa ikitoa pembejeo za ruzuku kwa wakulima.