Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Same, Azza Karisha, amewahimiza vijana kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akizungumza wakati wa ziara ya utekelezaji katika Kata za Bwambo, Mpinji, na Myamba katika Jimbo la Same Mashariki, Karisha alisisitiza umuhimu wa vijana kujitokeza na kushiriki katika uchaguzi huo.
Katika ziara hiyo,Karisha amefanikiwa kugawa kadi kwa wanachama wapya 105 ambao wamemua kujiunga na chama hicho ili kummunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuleta maendeleo, hususan katika Jimbo la Same Mashariki,kwani limekuwa ni chachu ya maendeleo katika Kata za Kalemawe, Kihurio, na Bendera.
Pia amewakikishia vijana kuhusu suala la mikopo kutoka Almashauri. Ingawa zoezi hilo lilisitishwa kwa muda, sasa limeboreshwa, na vijana waliojisajili na wenye sifa watapata mikopo. Ni muhimu kuhakikisha kuwa mikopo inarejeshwa kwa wakati ili wengine waweze kupatiwa.
“Pamoja na hayo yote niwatoe hofu vijana kuhusu swala la mikopo kutoka Almashauri Kwa Sasa zoezi Hilo lilisitishwa na Sasa hivi limeboreshwa hivyo pindi linaporudi Kwa wale vijanawaliojisajili na wenye sifa tutawasaidia kupata mikopo hiyo Kwa Sasa hivi zoezi Hilo linaendelea Kwa Baadhi ya wilaya Kwa majaribio ambao watapata mikopo hiyo basi wahakikishe pia wanalejesha Kwa Wakati hili wengine waweze kupatiwa” amesema Karisha.
Mbali na hayo, baadhi ya vijana wa Jimbo la Same Mashariki wamemuomba Mhe. Mbunge wa Jimbo hilo, Anna Kilango, kuwasaidia kupata mipira ya michezo baada ya kumalizika kwa Mashindano ya Samia Cup.