Wachezaji wa timu ya Faru Dume FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kushiriki mashindano ya Parimatch Kitaa Cup 2024 kwenye uwanja wa Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Karume United FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kushiriki mashindano ya Parimatch Kitaa Cup 2024 kwenye uwanja wa Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Faru Dume na Karume United wakichuana katika mechi ya ufunguzi ya Parimatch Kitaa Cu 2024 kwenye uwanja wa Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama Cha soka cha Manispaa ya Temeke (TEFA), Ally Kamtande na Mkuu wa Masoko wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch, Levis Paul wakikagua timu ya Karume United kabla ya kuanza kwa mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya Parimatch Kitaa Cupn2024 kwenye uwanja wa Zakhiem, Mbagala.
Wachezaji wa Faru Dume na Karume United wakichuana wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Parimatch Kitaa Cup 2024 kwenye uwanja wa Zakhiem, MBA gala.
……………………
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Kampuni ya michezo yakubashiri ya Parimatch imezindua michuano maalum ijulikanayo kwa jina la Parimatch Kitaa Cup 2024 yenye lengo la kuinua na kundeleza vipaji katika mpira wa miguu.
Mashindano haya yanashirikisha jumla ya timu nane kutoka maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Levis Paul.
Paul alizitaja timu hizo kuwa ni Faru Dume, Karume FC, Kawe UTD, Makubuli FC, Kauzu FC, Namanga FC, Mpakani FC pamoja na Rangi tatu FC.
Katika mchezo wa ufunguzi, Faru Dume iliifunga timu ya katume United kwa mabao 2-0 wakati Kawe United iliichapa Makubuli kwa bao 1-0 na Kauzu ikiifungashia virago Namanga kwa mabao 2-0 kutinga nusu fainali ambayo itachezwa leo Jumapili kwenye viwanja hivyo hivyo.
Mshindi wa mashindano hayo ya siku mbili atazwadiwa sh1milioni na wa pili atapata sh500, 000. Pia kutakuwa na zawadi ya mshindi wa tatu ambayo ni mipira miwili katika mashindano hayo.
Kwa mujibu wa Paul, pia kutakuwa na zawadi ya mfungaji bora, golikipa bora pamoja na mchezaji bora wa kila mchezo.”Timu zote shiriki zimepewa jezi na mpira ambazo zinatumika katika mashindano na morali ya kila mchezaji ipo juu,” alisema Paul.
Alisema kuwa kampuni ya Parimatch imedhamiria kuchangia maendeleo ya michezo nchini kwa vitendo na hasa kwa timu za mitaani ambapo kuna wachezaji wengi wanaoweza kuleta mafanikio kwa klabu mbalimbali na timu ya Taifa.
“Kutokana na hilo, ndiyo maana tumeandaa mashindano haya ya muda mfupi, kusaidia vifaa vya michezo na kuweka zawadi nono, hii itasaidia wachezaji kupambania timu zao ili kuibuka washindi.
Nawaomba mashabiki wa soka wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi ili kupata burudani safi kutoka timu zetu za mitaani, “alisema.
Kampuni ya Parimatch ni kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya ukaribisho ya asilimia 125 hadi kufikia Sh 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nao.
Parimatch imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.