*Mahakama ya Rufaa chini ya Majaji Rehema Mkuye, Abraham Mwampashi na Zainab Muruke yafutilia mbali hukumu ya Mahakama kuu divisheni ya biashara iliyoipa ushindi kampuni ya State Oil dhidi ya benki ya Equity
*State Oil walikopa Dola milioni 18 za kimarekani sawa wastani wa Shilingi bilioni 45 za Kitanzania kwa kampuni ya Dubai wakidhaminiwa na benki hiyo iliyotoa ‘Special Letter of Credit’
*Ikatumia mkopo huo kufuta madeni yao katika mabenki mengine yaliyokuwa yanawadai na kiasi kingine kuongezea mtaji
*Ulipofika wakati wa kulipa ikakataa kulipa mkopeshaji akambana mdhamini na kutumia ‘Special Letter of Credit’ aliyoweka kulipwa mabilioni aliyokopesha
*Mkopeshswaji alipofatwa na mdhamini aliyelipishwa mabilioni kwa niaba yake akakataa kulipa na kukimbilia mahakamani na Jaji Magoiga akampa ushindi katika hukumu iliyojaa utata
* Mahakama ya Rufaa sasa yaagiza shauri hilo lianze kusikilizwa upya katika Mahakam ya Biashara
* Kwa hukumu hiyo sasa benki inaweza kuendelea na taratibu za kurejesha amana yake kutokana na dhamana zilzowekwa na kampuni hiyo
* Wanufaika wengine wa Mikopo chechefu waliokopa na kukimbilia mahakamani sasa matumbo joto, wahaha kujisafisha bila mafanikio
* Jamvi la Habari lapongezwa kusimama kidete kufichua madudu yaliyofanywa na ‘ushirika chechefu’ ya kukataa kulipa mikopo kutumia Mahakama
Na. Mwandishi wetu,
Mahakama ya Rufaa imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama kuu divisheni ya biashara katika moja ya kesi maarufu za mikopo chechefu baina ya kampuni ya State Oil dhidi ya Benki ya Equity kesi ambayo Mahakama Kuu hiyo chini ya Jaji Magoiga iliipa ushindi kampuni ya husika ambayo ilikopa dola milioni 18 (zaidi ya Shilingi Bilioni 45 za kitanzania) na kukataa kulipa kisha kukimbilia mahakamani
Ikiongozwa na majaji watatu Rehema Mkuye, Abraham Mwampashi na Zainab Muruke mahakama hiyo imeona kasoro kadhaa za kiuendeshaji wa kesi katika mahakama kuu divisheni ya biashara iliyofunguliwa na kampuni ya State Oil ikitaka mahakama itoe amri kwa kampuni hiyo kutokulipa kiasi cha shilingi bilioni 45 za kitanzania ilizokopa kwa kampuni ya Lamar ya Dubai na kudhaminiwa na benki ya Equty
Katika hukumu hiyo ambayo gazeti hili imepata nakala yake, majaji hao wanasema kuwa wametumia mamlaka waliyopewa kisheria ya kufuta hukumu na mwenendo mzima wa kesi hiyo na kuelekeza ianze kusikilizwa upya katika mahakama kuu divisheni ya biashara huku ikionyesha makosa kadhaa kubwa likiwa ni kutokushirikishwa kwa upande muhimu katika shauri hilo la Equity Benki ya Kenya
‘’Kiasi cha mkopo cha USD 18,640.000.00 kilitolewa na LAMAR kwa SOT(State Oil Tanzania) kupitia akaunti ya escrow iliyofunguliwa na EBK (Equity Bank Kenya) kwa jina lake. Baada ya hapo, EBK ililipa deni lote la SOT kwa EBT na benki zingine. EBK pia ilijilipa kamisheni ya USD 372,800.00 yenyewe, USD 750,000.00 kwa NISK kwa huduma za ushauri na udalali na USD 74,560.00 kwa serikali ya Kenya kama ushuru wa bidhaa na Salio lililosalia kwa SOT lilikuwa USD 736,899.74.’’ Inasomeka sehemu ya Hukumu hiyo
Inaelezwa kwamba hati ya madai ya mjibu maombi Katika shauri la Msingi Mahakama Kuu haikufanyiwa marekebisho baada ya Mahakamu Kuu kutoa uamuzi wa kuunganisha EBK kuwa sehemu ya kesi baada ya EBK kuwa sehemu ya kesi Jaji aliyesikiliza shauri alijielekeza isivyo kwa kushindwa kutoa amri ya mleta Madai SOT kufanya marekebisho ya hati yake ya Madai ili kuweza kuunganisha Madai dhidi ya EBK kwa minajili ya haki.
Hata hivyo Mawakili wa pande zote hawakuona kama ilikuwa ni Makosa makubwa kwa Mahakama kuu kushindwa kutoa amri ya marekebisho ya Hati ya Madai.
Mahakama ya Rufaani kwa mamlaka yake yenyewe imeona Zaidi