HALMASHAURI ya Mji Mafinga wameanza kutoa elimu ya Mpiga Kura kwa wawakilishi wa Wananchi wa Makundi ya Wazee,Vijana, Wanawake,Watu wenye Mahitaji Maalumu, Boda boda na vikundi vya Bajaji kwa lengo likiwa ni kuwajengea uwezo makundi hayo katika kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akizungumza Mratibu wa Uchaguzi Halmashauri ya Mji Mafinga Raineli Pius Mwenda alisema kuwa Makundi yanayopatiwa Elimu ya Mpiga Kura ni kutoka katika Kata za Upendo, Wambi,Changarawe, Boma na Kinyanambo.
Mwenda amesema jumla ya Mada 6 kuhusu Elimu ya Mpiga Kura zitatolewa ikiwemo mada ya Sheria zinazosimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Elimu ya MpigaKura,Utaratibu wa Uchaguzi,Maadili na Rushwa katika Uchaguzi na Uragibishaji na Uhamasishaji.
Kwa upande wake Muwezeshaji Ndugu, Benedict Kibiki alisema kuwa Sheria zinazosimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ilitolewa kwa siku mbili katika Ofisi ya Kata ya Boma na inashirikisha washiriki 50 kutoka katika kata 5 kati ya 9 za Halmashauri ya Mji Mafinga.