Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Frank Nyabundege (kushoto) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fedha Benki ya Exim Bw. Shan Kinswaga (kulia) wakisani mkataba wa makubaliano na Benki ya Exim kutoa dhamana ya mikopo ya jumla ya Shilingi bilioni 30 kwenye minyororo wa thamani ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kipindi cha miaka mitano katika hafla fupi iliyofanyika leo Mei 16, 2024 katika ofisi za makao Makuu benki ya TADB, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Frank Nyabundege (kushoto) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Fedha Benki ya Exim Bw. Shan Kinswaga wakishika mkataba ya makubaliano baada ya kusaini.
Mkuu wa Kitengo cha Sheria Benki ya TADB Dkt. Edson Rwechungura (kushoto) pamoja na Mwanasheria Mkuu Benki ya Exim Bw. Edmund Mwasaga (kulia) wakisani mkataba wa makubaliano na Benki ya Exim kutoa dhamana ya mikopo ya jumla ya Shilingi bilioni 30 kwenye minyororo wa thamani ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kipindi cha miaka mitano katika hafla fupi iliyofanyika leo Mei 16, 2024 katika ofisi za makao Makuu y benki ya TADB, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Frank Nyabundege akizungumza na waandishi wa habari kuhusu muhimu wa kuingia makubaliano na Benki ya Exim kwa ajili ya kutoa dhamana ya mikopo kwa wakulima.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Fedha Benki ya Exim Bw. Shan Kinswaga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kuingia makubaliano na benki ya TABD kwa ajili ya kutoa mikopo kwa walimu.
Meneja wa Mfuko wa Dhamana, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. George Nyamrunda akizungumza jambo katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano na Benki ya Exim kutoa dhamana ya mikopo ya jumla ya Shilingi bilioni 30 kwenye minyororo wa thamani ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kipindi cha miaka mitano iliyofanyika leo Mei 16, 2024 katika ofisi za makao Makuu benki ya TADB, Dar es Salaam.
………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia Mfuko wa Dhamana wa Wakulima Wadogo (SCGS – Small holder Credit Guarantee Scheme) imeingia makubaliano na Benki ya Exim kutoa dhamana ya mikopo ya jumla ya Shilingi bilioni 30 kwenye minyororo wa thamani ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kipindi cha miaka mitano.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 16, 2024 jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kusaini Mkataba wa makubaliano kati ya TADB na Benki ya Exim, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB Bw. Frank Nyabundege, amesema kuwa hatua hiyo itaiwezesha TADB kuchangiza upatikanaji wa mitaji kwa wakulimu kupitia benki ya Exim.
Bw. Nyabundege amesema kuwa benki ya Exim itakuwa inatoa mikopo kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo, mifugo na uvuvi ambapo TADB imetoa dhamana ya hadi asilimia 70 kwa mikopo yote hususani kwa vijana, wanawake pamoja na miradi inayosaidia kupunguza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
“Wachakataji wadogo na wakati, wakulima wadogo wa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi wataendelea kunufaika kupitia ushirikiano huu kwa mikopo itakayotolewa na benki ya Exim nchini” amesema Bw. Nyabundege.
Amesema kuwa benki ya TADB inatambua changamoto ya mitaji na upatikanaji wa mikopo nafuu inayowakabili wakulima nchini, hivyo makabaliano na benki ya Exim inakwenda kuongeza nguzvu na ushirikiano ili kutoa mikopo kwenye sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Amefafanua kuwa kwa muda mrefu wakulima wamekuwa wakipata changamoto ya mitaji, huku wengine wakilazimika kukopa kwa masharti magumu na riba kubwa.
“Tuna jukumu la kuhamasisha na kuwawezesha mabenki na taasisi za kifedha nchini kama benki ya Exim ili kuwasaidia wakulima kupata mitaji na kujikwamua kiuchumi” amesema Bw. Nyabundege.
Amesema kuwa ili kuogeza wigo benki ya TADB imefanya maboresho na kuongeza kiwango cha dhamana kutoka asilimia 50 mpaka kufikia 70 kwa miradi ya wanawake, vijana na miradi inayosaidia kupunguza au kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Bw. Nyabundege ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha TADB kutimiza majukumu yake, huku akitoa wito kwa benki na taasisi za fedha kuendeleza ushirikiano ili kuleta tija kwa Taifa.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Fedha Benki ya Exim Bw. Shan Kinswaga, ametoa wito kwa wakulima na wadau kuchangamkia fursa ya kupata mikopo kwa ajili ya shughulia ya kilimo ambayo itapatikana katika matawi yote ya benki hiyo Tanzania Bara na Zanzibar.
Mpaka sasa Benki ya TADB imeingia makubaliano na taasisi za fedha 17 ambazo ni benki za biashara, kijamii, na taasisi ndogo za fedha zenye uwezo wa kuhudumia wakulima kupitia mtandao wa matawi zaidi ya 700 nchini.
Hadi kufikia Aprili 2024 jumla ya mikopo iliyodhaminiwa na TADB kupitia SCGS imefikia shilling bilioni 300, huku wanufaika wa moja kwa moja 23, 940 na wanufaika wasio wa moja kwa moja 897, 900 kutoka mikoa 27 na Wilaya 129 Tanzania Bara na Visiwani Zanzabar.