Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Paul Makonda akipokea pikipiki hizo mkoani Arusha leo
…….
Happy Lazaro, Arusha
Katika kuhakikisha ulinzi unazidi kuimarika mkoani Arusha na utalii kuendelea kupaa zaidi,Benki ya CRDB imekabidhi pikipiki 20 zenye thamani ya sh,milioni 150 kwa mkoa wa Arusha.
Uwepo wa pipikipiki hizo utasaidia sana kuimarisha ulinzi na usalama kwa mkoa wa Arusha ,ambapo benki hiyo.imekuwa ikifanya hivyo kama njia ya kurudisha kile kilichopatikana kwenye jamii.
Akizungumzia tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, AbdulMajid Nsekela amesema msaada huo umekuja kupitia mpango wa benki hiyo wa kutenga asilimia 1 ya faida inayoipata kila mwaka kwa ajili la kurejesha kwa jamii kupitia sekta ya elimu,Afya .
Amesema kila mwaka benki hiyo imekuwa ikifanya mkutano ukitanguliwa na mkutano wa wanahisa ambao huenda sanjari na kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo kukabidhi Madawati ujenzi wa madawati ikiwa ni mpango wa kuunga mkono juhudi za Raisi Samia Suluhu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ambaye ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuunga mkono adhma ya mkoa huo ya kuhakikisha kuwa usalama upo wakati wote ikiwa ni sehemu ya kuchagiza ukuaji wa utalii.
Amesisiitiza kuwa nyenzo hizo walizokabidhiwa leo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuimarisha doria maeneo mbalimbali ili kuhakikisha watalii wanaotembelea Arusha wanabaki salama mpaka muda wao wa kuondoka.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo ameishukuru benki hiyo ya CRDB kwa msaada huo akidai kuwa wapo macho kuhakikisha wanalinda raia na mali zao usoku na mchana ikiwemo watalii wanaotembelea Mji wa Arusha.