*Akagua barabara ya kibada Mwasonga,
*Atembelea Kiwanda cha Nyati Cement.
*Afanya Mkutano wa hadhara eneo la Kijaka-Kimbiji
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 15, 2024 amefanya ziara ya kimkakati Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila alianza ziara yake kwa kukagua miundombinu ya TANROAD hususani barabara ya Kibada Mwasonga ambapo amesema Serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan iko katika hatua ya kujenga barabara hiyo KM 51 kwa kiwango cha lami kwa masilahi mapana ya wananchi na uwekezaji ulioko katika maeneo hayo.
Aidha RC Chalamila akiwa mwasonga magengeni alipata wasaa wa kuwasikiliza wananchi waliomsimamisha kueleza kero zao, papo hapo aliweza kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ya Ardhi na Afya ambapo aliweza kumpatia Mwananchi mmoja shilingi *milioni 2* ambaye alilalamika kutapeliwa kiasi hicho na mtu licha ya makubaliono yao kufanyika katika ofisi ya Serikali ya Kata na Mtaa ” Natoa pesa yangu itakapofika saa 12:00 jioni leo Viongozi wa Serikali ya Kata leteni pesa yangu” Alisema RC Chalamila
Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa akitembelea kiwanda cha Nyati Cement kujionea uwekezaji uliofanyika ambapo amewataka kutunza mazingira, kuongeza uzalishaji wa saruji lakini pia kiwanda kitoe CSR katika ‘National level’ na sio ‘local’ tu Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji ikiwemo kuhakikisha kuna umeme wa uhakika na barabara nzuri
Sanjari na hilo RC Chalamila alifanya Mkutano wa hadhara katika eneo la Kijaka-Kimbiji ambako kuna mgogoro mkubwa kati ya Wananchi na Jeshi la Wananchi JWTZ, Mhe Mkuu wa Mkoa amewasikiliza Wananchi na upande wa Jeshi ambapo ameahidi kurudi tena huku akiwataka wananchi kutulia ” Tutafuatilia nyaraka kama eneo litaonekana ni la Jeshi la Wananchi Tanzania watapewa na Kama eneo litaonekana la wananchi watapatiwa ” Alisema RC Chalamila.
Katika Ziara hiyo RC Chalamila aliambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Halima Bulembo, wataalam kutoka TARURA na TANROAD,na wataalam wengine kutoka ofisi yake na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.