Mkaguzi kata ya Oloipiri Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha Mkaguzi msaidizi wa Polisi A/INSP Paschal Kiango ameiomba Jamii ya kifugaji katika kata hiyo kupokea dhana ya ulinzi Jirani ambayo itasaidia kupunguza uhalifu na kubadilisha taarifa pindi uhalifu unapotokea katika eneo hilo.
Mkaguzi huyo amebainisha hilo alipokutana na mwananchi wa kitongoji cha Orangai ambapo alimuomba Bwana Kusaleti Simoni kuwa balozi wa Ulinzi Jirani ambao utawasaidia wao kama Jamii ya kifugaji kukabiliana na uhalifu pindi unapotokea katika kata hiyo.
Mkaguzi huyo Pia amemwambia mwananchi huyo kuwa endapo watatumia njia hiyo watambue kuwa mifugo yao na wao watakuwa salama.
Vilevile amewataka kutambua na kuelewa vyema dhana ya mazizi salama ambayo yataweka mazingira bora na salama kwa mifugo yao ambayo itakuwa salama wakati wote.
Sambamba na hilo amemuomba kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilayani humo kwa kutoa taarifa za wahalifu wanaojihusisha na wizi wa mifugo.