Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Elke Wisch, ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni jijini Dodoma, Mei 14, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Elke Wisch kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni jijini Dodoma, Mei 14, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Elke Wisch kuhusu machapisho mbalimbali ya shirika hilo baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni jijini Dodoma, Mei 14, 2024. (Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya mazao na bidhaa mbalimbali yanayosindikwa na kutengenezwa Tanzania baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma, Mei 14, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Elke Wisch (wa tatu kushoto) baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, bungeni jijini Dodoma, Mei 14, 2014. Wengine ni Maofisa kutoka UNICEF. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Elke Wisch baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma, Mei 14, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Mei 14, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) Elke Wisch, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni Jijini Dodoma.
Katika mazungumzo yao Mheshimiwa Waziri Mkuu amemuahidi Bi. Wisch kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kulipa ushirikiano Shirika hilo ili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, maji na elimu.
Kwa upande wake, Bi. Wisch ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuweka mipango katika kuboresha sekta ya elimu, mpango wa kukabiliana na maafa pamoja na kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha, Bi. Wisch ameahidi shirika hilo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuandaa na kutekeleza mpango kazi wa kukabiliana na maafa.