Viongozi Nyakika na Bweranyange waonywa kutokuwa Chanzo Migorogoro ya Wakulima na Wafugaji Karagwe.
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Abdallah Nyandular akiwa na wakaguzi Kata wa Nyakakika na Bweranyange Wilayani humo wamewataka viongozi wa kata hizo kutokuwa Chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji.
SSP Nyandular amewaambia hatopenda kusikia migogoro ya wakulima na wafugaji ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo kupitia kikosi cha Kuzuia wizi wa mifugo STPU wamekuwa wakitoa elimu Kwa makundi ya wakulima na Wafungaji juu ya Matumizi bora ya ardhi ili kuzuia muingiliano wawakulima na wafugaji.
Aidha amewambia viongozi hao kuwa wanaowajibu kisheria kutoa Elimu Kwa wananchi wao Juu ya matumizi bora ya ardhi.
Nae Mkaguzi kata wa kata ya Nyakakika Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Olipa Chitongo amewataka viongozi wa kata yake kufuata taratibu za kisheria endapo wanapata changamoto.
Pia amewaomba viongozi wa kata hiyo kutambua kuwa kiongozi ni kiunganishi kati ya Serikali na wananchi katika kutatua changamoto zozote zile kata hiyo.