Akieleza kuhusu zoezi hilo la serikali Flugence Kanuti ambaye ni kamishina wa ardhi msaidizi Njombe amesema wamiliki wote wanatakiwa kufika katika ofisi za halmashauri au ofisi ya ardhi mkoa ili kupata ankara za kulipa kodi hiyo na kisha kuweka bayana namna kodi hiyo inaweza kulipwa kupitia simu ya kiganjani.Kanuti amesema punde baada ya muda wa siku 30 kukamilika ,wale wote ambao watakuwa hajalipa kodi hiyo wataanza kufatiliwa na kisha kufikishwa mahakamani ili kupata amri ya kuuza mali zao kwa muongozi wa sheria ya ardhi no.50 ,1999 ili kuokoa upotevu wa kodi hiyo ya serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Kodi hii ni tofauti na kodi ya majengo hivyo wamiliki wote wa viwanja na mashamba mnapaswa kulipa kodi zenu ndani ya muda uliyopangwa,alisema Flugence Kanuti “
Katika hatua nyingine kamishina wa ardhi msaidizi mkoa wa Njombe 2023 ofisi ya ardhi ya mkoa wa Njombe Flugence Kanuti amesema walipewa lengo la kukusanya bil 4 lakini hadi mwaka unaisha kiasi kilichokusanywa kilikuwa ni Bil 1.2 ambacho ni sawa na asilimia 26 ambacho ni kidogo na kisha kuweka wazi sababu ya makusanyo hafifu kuwa ni mwamko mdogo wa wananchi kulipa kodi.
“Ili kuongeza mwamko wa watu kulipa kodi ili kufikia lengo la mwaka 2024 la kukusanya bil 4 za mapato ambayo hadi sasa imekusanywa asilimia 22 wanakwenda kupita mlango kwa mlango kuhamasisha,vyombo vya habari na mabango,alisema kamishina wa ardhi msaidizi Njombe Flugenzi Kanuti”
Baada ya kutolewa kwa tangazo hilo la siku 30 za kulipa kodi ya viwanja na mashamba kwa wamiliki wa mali hizo ,mtandao huu umeongea na baadhi ya wakazi wa Njombe akiwemo Agripina Mtweve ambae anasema idadi kubwa ya wananchi hawana uelewa wowote kuhusu kodi ya viwanja,Mashamba na Majengo hivyo kupitia elimu za mara kwa mara wameendelea kujengewa uelewa na kuonyesha moyo wa kwenda kulipa.
“Kiukweli tulikuwa hatujui chochote lakini kuanzia sasa nawahamasisha watanzania wenzangu kwenda kulipa kodi za serikali ili zitumike kutekeleza miradi ya maendeleo nchini,alisema Agripina Mtweve”