Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi mbalimbali, wadau wa Nishati pamoja na Washiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024. Rais Samia pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo wa Kimataifa ambao umewakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali Duniani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jonas Gahr Støre kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Wenyeviti Wenza, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jonas Gahr Støre wa pili kutoka kulia, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wa kwanza kulia wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wenyeviti Wenza, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Jonas Gahr Støre wa pili kutoka kulia, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wa kwanza kulia pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Nishati (IEA) Mhe. Dkt. Fatih Birol wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024.
Viongozi, Wadau wa Nishati pamoja na Washiriki mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Afrika uliofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO Jijini Paris nchini Ufaransa tarehe 14 Mei, 2024