Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wasita kulia) akimkabidhi funguo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,John Masunga(wanne kulia), wakati wa Hafla ya Makabidhiano ya Magari 12 ya Uokozi na Nyumba 6 za Ghorofa kwa ajili ya Makaazi ya Askari. Wapili kulia ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo(wanne kushoto),Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ally Senga Gugu(watatu kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama,Vita Kawawa(watatu kushoto).Hafla hiyo imefanyika eneo la Kikombo,jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Nyumba 6 za ghorofa kwa ajili ya makaazi ya askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Daniel Sillo,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Dodoma, Kamarade Adam Kimbisa na kutoka kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga,Waziri wa Madini,Anthony Mavunde,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama,Vita Kawawa .Hafla hiyo imefanyika eneo la Kikombo,jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipata maelezo ya gari maalumu la uokozi kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi,Mhandisi Issa Omary(kushoto) wakati wa Hafla ya Kukabidhi magari 12 na nyumba 6 za ghorofa za Makaazi ya Askari yaliyopo eneo la Kikombo.Kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,John Masunga hiyo imefanyika eneo la Kikombo,jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi Waziri wa Madini,Anthony Mavunde ambae pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini mfano wa funguo wa magari 12 ambapo gari moja limetolewa kwa mkoa wa Dodoma ikiwa ni mkakati wa serikali kukabiliana na majanga mbalimbali.Wengine kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama,Vita Kawawa,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo na kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,John Masunga.Hafla hiyo ya makabidhiano ya magari 12 na ufunguzi wa nyumba 6 za ghorofa imefanyika eneo la Kikombo jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiendesha moja ya magari 12 aliyokabidhi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya shughuli za uokozi,wakati wa Hafla ya Kukabidhi magari 12 na nyumba 6 za ghorofa za Makaazi ya Askari yaliyopo eneo la Kikombo.Hafla hiyo imefanyika eneo la Kikombo,jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi