Mkurugenzi wa Shughuli za Baraza la Wawakilishi Othman Ali Haji akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Taarifa ya Shughuli za Mkutano wa Kumi na Tano wa Baraza la Kumi la Wawakilishi ambalo linatarajiwa Kuanza Jumatano 15Mei 2024 hadi tarehe 28 Jun,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar. Mwandishi wa Habari wa Furaha FM Yahya Swaleh akiuliza maswali katika Mkutano wa Mkurugenzi wa Shughuli za Baraza la Wawakilishi Othman Ali Haji wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Taarifa ya Shughuli za Mkutano wa Kumi na Tano wa Baraza la Kumi la Wawakilishi ambalo linatarajiwa Kuanza Jumatano 15Mei 2024 hadi tarehe 28 Jun,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar. Mkurugenzi wa Shughuli za Baraza la Wawakilishi Othman Ali Haji akijibu Maswali ya Waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa kuhusiana na Shughuli za Mkutano wa Kumi na Tano wa Baraza la Kumi la Wawakilishi ambalo linatarajiwa Kuanza Jumatano 15Mei 2024 hadi tarehe 28 Jun,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
Afisa wa Habari wa Habari Maelezo Takdir Ali akiuliza maswali katika Mkutano wa Mkurugenzi wa Shughuli za Baraza la Wawakilishi Othman Ali Haji wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Taarifa ya Shughuli za Mkutano wa Kumi na Tano wa Baraza la Kumi la Wawakilishi ambalo linatarajiwa Kuanza Jumatano 15Mei 2024 hadi tarehe 28 Jun,hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza hilo Chukwani Zanzibar.
………………
Na Takdir Ali. Maelezo. 13.05.2024.Mkutano wa kumi na tano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar bajeti 2024/2025, unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 15 mwezi huu na kumalizika tarehe 28 Mei, 2024.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani, kwa niaba ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mkurugenzi wa shughuli la Baraza la Wawakilishi Othman Ali Haji amesema jumla ya Maswali ya msingi 291 yataulizwa katika mkutano huo.
Aidha amesema jumla ya miswada mitatu ya Sheria inatarajiwa kuwasilishwa, na mswada mmoja uliosomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa kumi na nne utajadiliwa katika na wajumbe wa Baraa la Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Ameitaja miswada hiyo kuwa ni pamoja na Mswada wa sheria ya Fedha, mswada wa sheria ya kuidhinisha matumizi ya Serikali kwa mwaka 2023/2024 na mswada wa sheria ya maerekebisho ya sheria mbalimbali na kuweka masharti bora ndani yake.
Hata hivyo amesema, Serikali kupitia Wizara ya Fedha imekuwa inatoa Mafunzo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ili kuweza kuwaongezea ujuzi wa utekelezaji wa majukumu yao.