Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Ubungo umepitia miradi mbalimbali ya maendeleo hakuna mradi uliokataliwa
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Wilaya ya Ubungo leo Mei 12,2024 umekimbizwa umbali wa KM 64.5 umetembelea, umekagua, umeweka jiwe la msingi, pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Tsh 306,917,122,909.99/=
Sanjari na hilo Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya hiyo umeendelea kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kupitia Ujumbe wa mbio hizo mwaka huu unaosema “Uhifadhi wa Mazingira na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pia Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge Uhuru katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya na Rushwa
Aidha miradi iliyopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika Wilaya ya Ubungo ni mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kinzudi, Ujenzi wa Shule Mpya ya msingi Kibamba B, Mradi wa Mfumo wa kusukuma maji Luguluni- DAWASA, Kikundi cha Urican Printing Sinza, Mradi wa Uhifadhi wa taka kwenye vizimba, kutembelea mradi wa huduma za jamii X – Ubungo, Kutembelea Ujenzi wa Madarasa Yusuf Makamba, Uzinduzi wa Kituo cha Afya Makuburi
Mwenge wa Uhuru 2024 katika Mkoa wa Dar es Salaam umekimbizwa katika Wilaya zote Tano ambapo Mbio hizo zimehitimishwa leo Mei 12,2024 katika Wilaya ya Ubungo kesho Mei 13, Mwenge wa Uhuru 2024 ukiongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg Godfrey Eliakimu Mnzava inatarajiwa kikabidhiwa Kusini Pemba na Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila.