Viongozi wa dini mbalimbali nchini na wazee wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia mmomonyoko wa maadili katika jamii na kuhakikisha mila na desturi za utamaduni wa mtanzania zinaendelea kustawi
Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati wa kikao chake na viongozi wa dini na wazee wa wilaya hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Monarch kata ya Kitangiri kwaajili ya kusikiliza kero na changamoto zao, kupokea ushauri juu ya utendaji wa Serikali, kuhamasisha maendeleo, kuhamasisha ushiriki wa uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapiga kura, kushiriki uchaguzi mkuu na Serikali za mitaa ambapo amewataka kukemea vitendo viovu katika jamii na kuchukua hatua kudhibiti kuporomoka kwa maadili
” SmaendeleSuala la maadili nyie ndio wataalam, Nyie ndio tunategemea muwe mstari wa mbele na watatuzi wa hili ” Alisema
Aidha Dkt Mabula mbali na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo akawahakikishia wazee hao kuwa Serikali inatambua mchango wao na kwamba itaendelea kutekeleza wajibu wake kuhakikisha jamii inazidi kuimarika
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la wazee wilaya ya Ilemela shekh Mohamed Yusuph mbali na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kazi nzuri anayoifanya ameongeza kuwa wazee wa wilaya ya Ilemela wanaridhishwa na utendaji wa Mbunge wa Jimbo hilo na kwamba wataendelea kumuunga mkono kuhakikisha Jimbo hilo linazidi kupata maendeleo kwani kazi kubwa imefanyika katika kipindi cha uongozi wa Mbunge Dkt Angeline Mabula huku akiahidi kushirikiana na wazee wengine katika kuzuia mmomonyoko wa maadili katika jamii
Joshua F. Arwa ni makamo askofu wa kanisa la Deliverance ambapo licha ya kumpongeza Mbunge huyo akawataka viongozi wa dini na wazee kuendelea kumsaidia Mbunge huyo katika kujenga jamii yenye ustawi na kuwa mstari wa mbele kumshauri ili wananchi waweze kupata maendeleo
Mbunge Dkt Angeline Mabula yupo jimboni Kwa ziara za kawaida akikutana na makundi mbalimbali kusikiliza kero na changamoto zao