Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa ametembelea Mashamba ya Vijana wa (BBT) Building a Better Tomorrow yanayopatikana Chinangali Dodoma akipokelewa na Mratibu wa Mradi Ndugu Vumilia Kankuba pamoja na Viongozi wengine.
Mhe Kissa akiwa Chinangali amesema Aliyokuwa na asikia na uhalisia ni tofauti Serikali imewekeza sana Kwa Vijana kwenye hili la BBT lazima tumpongeze Mhe Rais Dkt Samia suluhu Hassan pamoja na wizara ya Kilimo ikiongozwa na Mhe Hussein Bashe na timu yake, ukiangalia hapa Mazao yamekubali ikiwemo zao la Alizeti zaidi hekta 100 zimekubali .
” _Hongereni Kwakweli dada Vumilia Mratibu Mkuu na wenzako pamoja na Wizara mmefanya jambo kubwa la kupongezwa Vijana wamepambana_ “.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe Kissa amefika Chinangali kujionea Uwezekaji wa Vijana pamoja na kujifunza changamoto na uwezekano wa kuianzisha Njombe na tayari Vijana wanasubiri Uwanzishwaji wa (BBT) Building a Better Tomorrow .
Nae Mratibu Mkuu wa Building a Better Tomorrow (BBT) Ndugu Vumilia Kankuba amefurahi sana Ujio wa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kufika Mashamba ya Vijana Chinangali kujionea uwekezaji na kusema wapo tayari kuanzisha BBT Wilaya ya Njombe.