Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na akimvalisha Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson medali ya ushiriki wa mbio za Mbeya Tulia Marathon 2024 zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Mei 11, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………….,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 11, 2024 ameshiriki katika tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathoni 2024 zilizoandaliwa na Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Tulia Trust. Mbio hizo zilianzia na kuishia kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Mei 11, 2024.
Baadhi ya viongozi walioshiriki mbio hizo ni Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma, Wakuu wa Mikoa ya Njombe na Mbeya, Wabunge na Viongozi wa Vyama vya Siasa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa wakishiriki katika tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathon 2024 zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Mei 11, 2024. Wa pili kushoto ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathon 2024 zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Mei 11, 2024. Kulia kwake ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson, kulia ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipongezana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge baada ya kumaliza mbio za Kilomita tano aliposhiriki mbio za Mbeya Tulia Marathon 2024 zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Mei 11, 2024. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika tukio la mbio za Mbeya Tulia Marathon 2024 zilizoanzia na kuishia kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Mei 11, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)