Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta Stella Sarakikya (kushoto) akimkabidhi Madaftari Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kunduchi Mwajabu Bakari kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wahitaji wa Shule hiyo wakati walipotembelea leo Mei 11, 2024 iliyopo Kata ya Tegeta jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta wakitoa msaada wa vifaa mbalimbali vya Shule kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kunduchi wakati walipotembelea shule hiyo leo Mei 11, 2024 jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kunduchi wakishiriki michezo mbalimbali leo Mei 11, 2024 jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta wakifanya usafi katika shule ya Msingi Kunduchi iliyopo Kata ya Tegeta jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta wakifanya usafi katika Zahanati ya Tegeta jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta wakifanya usafi katika chuo hicho.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta wakiwa katika picha ya pamoja.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kunduchi iliyopo Kata ya Tegeta wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupewa zawadi ya madaftari, kalama, penseli, ufutio, shati la shule na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta wakibeba mabox ya Madaftari kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wahitaji wa Shule ya Msingi Kunduchi.
………
NAOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta leo Mei 11, 2024 wametembelea Shule ya Msingi Kunduchi iliyopo Kata ya Tegeta pamoja na Zahanati ya Tegeta kwa ajili ya kufanya matendo ya huruma ikiwemo kusafisha mazingira pamoja na kutoa vifaa vya shule kwa wahitaji.
Wakiwa katika Shule ya Msingi Kunduchi Wanafunzi hao wa Shahada ya Awali fani ya Utawala wa Umma na ya Uhasibu na Fedha wameshiriki na wanafunzi wa Shule hiyo michezo mbalimbali, kufanya usafi eneo la Shule pamoja na kutoa mahitaji ya vifaa vya Shule ikiwemo Daftari, mashati ya Shule, kalama pamoja na penseli.
Akizungumzia tukio hilo Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Kituo Cha Tegeta Bi. Stella Sarakikya, amesema kuwa wamefanikiwa kutoa vifaa vya shule kwa ajili kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji wa Shule ya Msingi Kunduchi ili kuhakikisha wanasoma katika mazingira rafiki.
Bi.Sarakikya amesema kuwa lengo ni kuunga mkono jitihadi za Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na kuhakikisha mazingira ya Shule ya Msingi Kunduchi na Zahanati yanakuwa safi ili afya za watu ziendelee kuimalika na jamii kwa ujumla.
“Shule ya Msingi Kunduchi tumetoa mashati ya shule, madaftari, kalama, penseli zenye thamani ya shilingi Laki nane” amesema Sarakikya.
Amesema ni utaratibu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kutoa mahitaji, huku akitoa wito kwa wanafunzi kujitoa kwa ajili ya jamii kwani sio wetu wenye uwezo wa kupata mahitaji yote wakiwa Shuleni.
Sarakikya ameushukuru uongozi wa Chuo kwa kuwapa nafasi na kuwaruhusu kushiriki pamoja na kuwaunga mkono katika kufanikisha tukio hilo muhimu.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kunduchi Mwajabu Bakari amewashukuru wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa kushiriki kusafisha mazingira pamoja na kutoa mahitaji wa wanafunzi.
“Tumeshiriki pamoja na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kufanya mazoezi ya pamoja kuanzia saa 12:30 asubuhi, tumesafisha mazingira pamoja na kuwapatia watoto zawadi ya mashati ya shule, madaftari, kalama, penseli, vifutio pamoja na kutoa elimu ya namna ya kujiendeleza na kutimiza uwajibu wao kusafirisha mazingira yao” amesema Sarakikya.
Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitoa kwa ajili ya kuisaidia jamii ili kuleta tija kwa manufaa ya Taifa.