*Asema kuwa Serikali imeshatamka kuwa kila Jumamosi kuanzia saa 12- 3:00 asubuhi Barabara yote mpaka ng’ambo ya Tanzanite bridge kuanzia Coco Beach itafungwa ili Mwanadar es Salaam afanye mazoezi
*Ataja faida zitokanazo na mazoezi
-Ampongeza RC Chalamila kushiriki mazoezi hayo kila Jumamosi
-Awapongeza WASAFI na wote waliojitokeza kuunga mkono jitihada za Serikali
Katika Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam ambae pia ndio Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo yote kwa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba A. Nguvila Leo tarehe 11 Mei, 2024 ameungana na Wana Dar es Salaam kufanya mazoezi kwa lengo kubwa la kuepukana na maradhi yasiyoambukiza
Dkt. Nguvila ameyasema hayo Leo ikiwa ni siku ya Jumamosi ambapo Serikali ilitamka kuwa barabara ya Tanzanite Bridge kuanzia Coco Beach itafungwa kuanzia saa 12 mpaka saa 3 asubuhi ili kila Mwanadar es Salaam afanye mazoezi
Ras Nguvila amezitaja faida za mazoezi kuwa ni pamoja na kuwa na Afya Bora na Kuboresha ndoa zetu kwa kupunguza “cholestrol mwilini
Dkt. Nguvila amempongeza RC Chalamila kwa kuungana na WanaDar es Salaam kufanya mazoezi kila Jumamosi ikiwa ni katika kuunga Mkono jitihada za Serikali ili kupambana na maradhi yasiyoambukiza
Mwisho Ras Nguvila amewapongeza WASAFI na wote waliojitokeza kwa wingi kufanya mazoezi hayo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali kupambana na magonjwa hayo na Kisha kuwaahidi WASAFI kuungana nao kwa muda mwingi usiokuwa jumamosi
“Mazoezi ni Tiba na Kinga Dhidi ya maradhi yasiyoambukiza, hayachagui kijana au mzee tujitokeze kufanya mazoezi”