Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 katika Mkoa wa Dar es Salaam tayari umeshakimbizwa katika Wilaya tatu toka ukabidhiwe ndani ya Mkoa huo ambapo umetembelea, umekagua, kuweka jiwe la msingi na umezindua miradi mbalimbali ya maendeleo hadi sasa Mkoa unaendelea kufanya vizuri katika Wilaya ambazo tayari zimeshapitiwa na Mwenge huo
Katika Wilaya ya Kigamboni Mwenge wa Uhuru umekimbizwa umbali wa KM 101.5 ukipitia miradi 8 yenye thamani ya Tsh 28,398,029,772 miradi yote imepita hakuna mradi uliokataliwa.
Aidha katika Wilaya ya Kigamboni Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 licha ya kupitia miradi ya maendeleo umeendelea kuelimisha wananchi kupitia Ujumbe wa mwaka huu wa ” Uhifadhi wa Mazingira na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa” pia Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Lishe pamoja na Rushwa.
Sanjari na hilo miradi iliyopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Kigamboni ni Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira na maeneo tengefu ya misitu ya mikoko, Maradi wa Ujenzi wa jengo la matibabu ya wagonjwa wa kifua kikuu (MDR-TB), Ujenzi wa Barabara ya Chagani-Polisi KM 0.7 kiwango cha lami, Mradi wa Chuo cha maendeleo ya wananchi Kigamboni, Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa, Mradi wa kikundi cha wachapatoyo, mradi wa maji Kisarawe II kupitia visima virefu na Mradi wa Shule mpya ya Sekondari Lingato.
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Mei 11, 2024 zinaendelea kukimbizwa Katika Wilaya ya Kinondoni ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itapitiwa na Mwenge huo.