Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama aliyeshiriki katika Misa ya Kumbukumbu ya Hayati Camilius Bernad Membe iliyofanyika Leo kwenye kanisa la St. Joseph Posts jijini Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa Jabari baada ya Misa hiyo.
……………….
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama liyeshiriki katika Misa ya Kumbukumbu ya Hayati Camilius Bernad Membe iliyofanyika Leo kwenye kanisa la St. Joseph Posts jijini Dar es Salaam amesema Marehemu Membe amewaachia mambo mengi ya kumuenzi ikiwa ni pamoja na kupendana., kushirikiana, umoja na Uzalendo kwa taifa.
Msama ameyasema hayo baada ya lumalizika kwa misa takatifu ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kufariki kwa Waziri huyo wa zamani jijini Dar es Salaam mwaka mmoja uliopita ambapo alizikwa kijijini kwake Rondo mkoani Lindi
Msama amesema kama mtu wa karibu na familia hiyo ambayo alifanya nayo kazi kwa muda mrefu akimsaidia Marehemu Bernard Membe katika kazi za familia atendelea kuenzi mazuri yaliyofanywa na Maehemu Membe Mwanadiplomasia na kiongozi mwandamizi wa taifa wakati akiwa hai
Naye Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ambaye ameshiriki misa hiyo ya kumbukumbu ya mwakamoja amesema kiongozi huyo atazidi kukumbukwa kwa mengi ambayo aliyafanya katika Taifa la Tanzania akiwa kiongozi na mwanadiplomasia.
Akizungumza mara baada ya ibada ya misa hiyo Waziri Nape amesema mazuri mengi ambayo yalifanywa na kiongozi huyo yatabaki kuwa alama kubwa hivyo ni wajibu wa watanzania kuendelea kumuenzi kwa yale mazuri ambayo aliyafanya ,nchini na nje ya mipaka ya Tanzania.
Naye Mke wa Hayati Membe Bi.Dorcus Membe amesema kama familia wamezidi kuenzi na kukumbuka mambo makubwa ambayo aliyafanya na wataendelea kumkumbuka kila wakati,huku akitumia wasaa huo kuwaomba watanzania kuenzi yale mema aliyoyafanya huku baadhi ya waumini walioshiriki ibada hiyo wakitoa maneno ya faraja kwa familia na watanzania kwa ujumla.
Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye na mkewe wakishiriki katika Misa ya kumbukumbu ya Hayati Bernard Membe katika kanisa la St. Joseph jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza wakati katika Misa ya kumbukumbu ya Hayati Bernard Membe kwenye kanisa la St Joseph jijini Dar es salaam.
MNEC wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mkoa wa Mbeya Bw Richard Kasesela ni miongoni mwa viongozi walioshiriki katika Misa hiyo ya kumbukumbu ya Hayati Bernard Membe kwenye kanisa la St. Joseph jini I Dar es Salaam.