*Ataka Umoja, Kiasi, Umakini, Maadili na Itikadi katika kukuza Ushirikia Nchini
*Aagiza Waajiri kupeleke Makato ya wanachama kwenye Saccos
*Awataka Viongozi kuhamasisha matumizi ya kidigitali sambamba na Wanaushirika kuongeza Ushirikiano wa Kibiashara wao kwa wao
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila ametoa wito huo kwa Viongozi na Watendaji wa Ushirika kutumia Dhamana hiyo waliyopewa kwa Uaminifu na Weledi Mkubwa
RC Chalamila ameyasema hayo Jana katika ufunguzi wa Jukwaa la Ushirika la Mkoa wa Dar es Salaam lililofanyika katika Ukumbi wa Blue Sapphire- Mbezi Beach Dar es Salaam
Mhe. Chalamila amesema ili Ushirika uzidi kukua na kuimalika unapaswa kuwa na Umoja, Kiasi, Umakini, Maadili, na Itikadi
Aidhaa, Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa Ushirika ni Ushirikiano ulio salama zaidi kwa kuwa unadhibitiwa na Serikali hivyo ni vema Waajiri kupeleke makato ya wanachama wao kwenye Saccos ili yaweze kutekelezwa kwa wakati
Vile vile RC Chalamila amewataka Viongozi kuhamasisha matumizi ya kidigitali ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji pamoja na Mamlaka za kiusimamizi sambamba na kuongeza ushirikiano wa kibiashara wao kwa wao katika Mikopo na Masoko
Kwa upandea wake Mkuu wa Wilaya Ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amewataka Wanaushirika kuhamasisha zaidi kwenye Weledi, Juhudi na Uwekezaji
Naye Anjela Nalimi ambaye ni Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Dar es Salaam amesema Ushirika unaendelea kutoa mchango Mkubwa katika uchumi wetu katika nyanja za Mitaji, Ajira, Masoko, Uzalishaji, Makazi na Kadhalika.