Chris Diaz aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Adili group
Na Hellen Mtereko, Mwanza
ALN Kenya,ALN Tanzania na ADILI Group yamteua Chris Diaz kuwa Mtendaji Mkuu wa ADILI na Mkurugenzi wa ukuaji na masoko mapya kwa makampuni.
Chris ametoa matokeo makubwa ya kibiashara na kuongoza mageuzi kwa mashirika yanayoongozwa ikiwa ni pamoja na Bidco Africa ambapo alihudumu kwa miaka 16.
Uteuzi wa Chris ni wa kimkakati na wakuimarisha utoaji wa huduma zilizounganishwa na mteja kwa njia mbalimbali za kibiashara ambapo hatua hiyo ya inalenga kukuza ushirikiano na kuendeleza teknolojia ya kisasa.
Kampuni ya Adili group ni Bora zaidi katika nafasi ya kukabiliana kwa haraka na mazingira yanayoendelea ya huduma za ushauri wa kisheria na kimkakati.
Aidha, Chris atatumia uzoefu wake kuwapa wateja maarifa na masuluhisho yanayohitajika ili kukabiliana na changamoto za Kampuni ikiwa ni pamoja na kusimamia usumbufu wa biashara sanjari na kuongoza mwelekeo wa kimkakati kwa kuzingatia kupanua wigo wa masoko yaliyopo na mapya na kuimarisha hadhi ya Adili group.