Mei 9, 2024 imefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi namba 11973/2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Tagha Komba wa Mahakama ya Wilaya ya Momba.
Mshtakiwa Mussa Ladislaus Twaha (Afisa Uvuvi Msaidizi Kata ya Kamsamba), mnamo 16.04.2017 na 03.06.2019 akiwa na nia ovu alitumia madaraka yake vibaya kinyume na k/f cha 31 cha PCCA Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022 kwa kushindwa aidha kupeleka fedha kwa Mhasibu wa H/W ya Momba au kuweka kwenye akaunti ya H/W hiyo kiasi cha shs 12,744,010/=.
Kosa hili ni kinyume na agizo namba 37(2) na 50(5) ya Randama ya Fedha ya Serikali ya Mtaa ya mwaka 2009 na hivyo kujipatia maslahi binafsi.
Pia, mshtakiwa anakabiliwa na kosa la Ufujaji na Ubadhirifu, kinyume na kifungu cha 28(1) cha PCCA Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2022 ambapo anatuhumiwa kufanya ubadhirifu wa Shs 12,744,010/= mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba zilizofika kwenye himaya yake akiwa mtumishi wa umma.
Kesi inaendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Hilda Mtaki.
Mshtakiwa amekana makosa yake na yupo rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Kesi itakuja Mahakamani Mei 16, 2024 kwa ajili ya hoja za awali.