Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na lishe (Nutrition International), ameshiriki katika vikao vya Bodi hiyo, Jijini Ottawa, Canada.
Shirika hili limekuwa na manufaa makubwa duniani na hasa nchi zinazoendelea. Kwa nchini Tanzania, Shirika hili kwa zaidi ya miaka 20 sasa, pamoja na mambo mengine, limekuwa likitoa msaada wa kiufundi na kiuendeshaji katika kupambana na utapiamlo – ikiwemo kutoa vidonge vya vitamini A kwa watoto wachanga ili kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.