Mei 08, 2024 zoezi la kuwaondoa tembo kwenye maeneo ya wananchi na kuwarejesha hifadhini kwa kutumia helikopta limeanza katika Wilaya ya Mbarali, jumla ya makundi matano (5) yenye tembo 43 yameondolewa kwenye maeneo ya wananchi katika Kata ya Igava na kurejeshwa Hifadhi ya Taifa Ruaha.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) Dkt. Eblate Ernest Mjingo amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kuhakikisha changamoto hiyo ya uvamizi wa tembo inatatuliwa ambapo timu ya wataalamu kutoka TAWIRI, TANAPA na TAWA ipo uwandani kuratibu zoezi hili.
Dkt. Mjingo amesema zoezi hilo litaendelea kwa siku ya kesho katika Kata nyingine za Wilaya ya Mbarali.