Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Wilbroad Mutafungwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Katunguru Wilaya ya Sengerema
Muonekano wa Jengo la Kituo cha Polisi Katunguru kinachojengwa na wananchi kwakushirikiana na Jeshi la Polisi
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Katunguru Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza wakiwa kwenye Mkutano
………….,…………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wananchi wa kata ya katunguru Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza wameshirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa kituo cha Polisi kilichoanzishwa kwa nguvu za wananchi.
Akizungumza Mei 7, 2024 alipotembelea na kukagua Maendeleo ya kituo hicho Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa amewahamasisha kumalizia ujenzi huo kwa wakati ili kiweze kuhudumia wananchi wa eneo hilo na maeneo jirani.
Aidha, kamanda Mutafungwa amechangia milioni moja na kuahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha kituo hicho kinakamilika na ili kianze kutoa huduma.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Katunguru Sadiki mola, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wananchi katika ujenzi wa kituo hicho
Naye, Mwenyekiti wa Kijiji cha Katunguru Lukas Lushoshaga, amesema ili Polisi wafanye kazi kwa uadilifu wanatakiwa kuwa na mazingira bora ya kufanyia kazi hivyo kituo kitakapo kamilika kitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Kata ya Katunguru na Kata za jirani.