Naibu Meya wa Jiji la Dodoma Asma Karama alikabidhi cheti kwa mmoja wa madereva bodaboda wa Jiji la Dodoma baada ya kupatiwa mafunzo ya elimu ya Usalama barabarani yaliyotolewa na Amend kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswisi
…………………
Na Mwandishi Wetu,Dodoma
UBALOZI wa Uswisi kwa kushirikiana na shirika la Amend wamekamiliaha awamu ya pili ya mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva wa pikipiki jijini Dodoma.
Katika awamu ya pili ya mafunzo hayo
madereva 145 wamepokea mafunzo hayo yalioanza Aprili 15 na kukamilika Mei 4 ndani ya Jiji la Dodoma ambapo Naibu Meya Asma Karama alikabidhi vyeti kwa madereva hao.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo ….. kutoka Shirika la Amend Simon Kalolo amesema hadi sasa, mradi huo wa usalama barabarani kwa vijana umewafikia madereva bodaboda wa 398 jijini Dodoma.
“Katika utekelezaji wa mafunzo haya, shirika la Amend linashirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, viongozi wa serikali za mitaa na shirika la Msalaba Mwekundu, linalowapatia madereva elimu muhimu ya huduma ya kwanza.
“Tunayofuraha tunapohitimisha awamu ya pili ya mafunzo haya hapa Dodoma, kuna mabadiliko makubwa kwani madereva wengi waliopatiwa mafunzo haya wanafahamu Sheria za usalama barabarani pamoja na alama zilizopo Kwetu hili tunasema ni hatua kubwa ya kusaidia kupunguza ajali kwa kundi hili,”amesema Kalolo.
Amefafanua kuwa madereva bodaboda waliohudhuria mafunzo hayo wamepatiwa vyeti vya ushiriki pamoja na viakisi mwanga vyenye jumbe mbalimbali wa usalama barabarani.
Ameongeza kuwa katika awamu ya kwanza ya mafunzo hayo, madereva 253 kutoka katika Kata mbalimbali za Jiji la Dodoma zikiwemo Kata ya Uhuru ambako mafunzo haya yamekuwa yakifanyika.
Kwa upande wake Mgeni rasmi wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo Naibu Meya Asma Karama amewasihi madereva bodaboda wote waliopata mafunzo kuwa mabalozi wazuri wa usalama barabarani katika maeneo yao kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Mafunzo haya ya usalama barabarani yaliambatana pia na kampeni ya usalama barabarani kwa vijana na watumiaji wengine wa barabara jijini Dodoma.