Na Sophia Kingimali.
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO )Mkoa wa Kinondoni Kaskazini imeendesha mjadala na wasomi wa chuo kikuu wanaosomea fani ya uhandisi wa umeme wenye lengo la kujenga uelewa kuhusu matumizi sahihi ya umeme majumbani.
Akizungumza wakati wa mjadala huo leo Mei 4,2024 jijini Dar es salaam hafisa uhusiano huduma kwa wateja wa shirika hilo mkoa wa Kinondoni Kaskazini Flaviana Mushi amesema mjadala huo umelenga kupata suluhusho la majanga ya umeme linalotokana na matumizi ya umeme majumbani.
“Leo tumeendesha mjadala huu na wasomi hawa wa chuo kikuu kwa sababu wao wanasoma taaluma hii ya uhandishi wa umeme lakini tunaamini kupitia wao wataweza kuelimisha umma mkubwa unaowazunguka”,Amesema
Amesema kufuatia majanga mbalimbali yanayotokea kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya umeme hivyo amewasihi wananchi kuhakikisha wanachukua taadhari pindi wanapotumia umeme kwenye matumizi ya nyumbani hata sehemu za uzalishaji mali.
Sambamba na hayo Mushi awehasihi wananchi kufuatia uwepo wa upepe mkali ukiotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa ‘Kimbunga HIDAYA’ wanapaswa kutosimama sehemu zenye miundombinu ya umeme kama nguzo hata kugusa nyaya zozote zitakazokuwa zimekatika badala yake watoe taarifa kwa kituo cha huduma kwa mteja ili waweze kutatua.
“Tumeona sasa hivi tunapita katika kipindi hiki cha upepe mkali tunapaswa kuchukua taadhari tukiona nguzo au nyaya za umeme popote tutoe taarifa na si kuzishika na kuzisogeza kwani kwa kufanya hivyo unahatarisha maisha yako”,Amesema.
Sambamba na hayo ameongeza kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu matumiza sahihi ya umeme kwenye nyumba ili kuhakikisha majanga yanayotokana na umeme majumbani yanakwisha kabisa.
Kwa upende wa mwakilishi kutoka shirika la Bima la taifa (NIC) ambao wameungana na TANESCO katika mjadala huo,Henry Mabula amesema pamoja na kuwa na matumizi sahihi ya umeme bado wananchi wanapaswa kujikinga kwa kukata bima ya majanga ya moto pindi majanga yanapotokea.
Amesema pamoja na kutolewa kwa ulimu sahihi ya matumizi ya umeme majumbani bado kunahaja ya kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya ukataji wa bima kama sehemu ya tahadhari.
“Tumekuja hapa kushirikiana na TANESCO kutoa elimu ya kujikinga na madhara yanayotokana na majanga ya moto yanayosababisha na umeme tunaamini kupitia nyinyi wasomi mtasaidia kupeleka elimu hii mbali na itawafikia watu wengi ili waweze kuchukua tahadhari dhidi ya majanga”,amesema Mabula.
Ameongeza kuwa bima ya moto inalipwa kutokana na thamani ya nyumba na gharama yake ikiwa ni ndogo kiasi ambacho mwa anchi anaweza kukata kwani kwa nyumba ya milioni 30 bima yake kwa mwaka ni shilingi 45000.
Nao baadhi ya wanafunzi wanaosomea fani ya umeme wameishauri TANESCO kuwakikisha wanatoa elimu ya matumizi sahihi ya umeme kwa kila mwananchi kwa kuwa wabunifu katika kutoa elimu hiyo ili iweze kumfikia kila mtu.
Wamesema elimu ikitolewa majanga ya umeme majumbani yataisha kwani watumiaji wengi wa umeme hawana elimu ya kutosha kuhusu umeme wanaoutumia badala yake mtu anaweza kufanya kitendo hatarishi na asigundua kama ni hatarishi kwa sababu ya kukusa elimu.