NIRC Dodoma
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeishukuru serikali kwa kuongeza bajeti kiasi cha shilingi bilioni 403 kutoka bilioni 373 kwa aajili utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji nchini.
Akizungumza katika viwanja vya bunge jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa amesema serikali kuongeza fedha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itasaidia kufikia malengo ya Taifa ya pato la asilimia kumi katika kilimo.
Aidha amesema Tume imejipanga kufanya utekelezaji ujenzi miundombinu ya umwagiliaji kwa kuwa na usimamizi madhubuti ikiwemo kufanya usanifu wa mabwawa zaidi ya 100 ili kuvuna maji kumsaidia mkulima kulima zaidi ya mara moja.
Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameipongeza Tume ya Taifa ya umwagiliaji kwa usimamizi madhubuti miradi ya umwagiliaji ambayo ipo kwenye utekelezaji na kukiri kuwa utekelezaji wa miradi hiyo itainua vipato vya wakulima kwa kuwa watalima kwa zaidi ya msimu mmoja wa kilimo.
Hata hivyo Bw. Raymond Mndolwa amesema kuwa uwekezaji unaofanywa na serikali katika Tume ya Taifa ya Umwagiliaji utaleta tija kwa wananchi kwa kuwa serikali inachimba visima kwenye halmashauri zote nchini pamoja na kuweka miundombinu ya umwagiliaji ili wakulima waweze kulima kwa mwaka mzima.