Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wageni kutoka nchini Sierra Leonne ambao walitembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali ya Sierra Leonne Dkt. Sartie Mohamed Kenneth.
Mganga Mkuu wa Serikali ya Sierra Leonne Dkt. Sartie Mohamed Kenneth akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya wajumbe kutoka nchini humo ambao walitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika.
Msimamizi wa wodi ya watoto ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Afisa Uuguzi Theresia Tarimo akiwaeleza wageni kutoka nchini Sierra Leonne huduma wanazozipata watoto waliolazwa katika wodi hiyo wakati wageni hao walitembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika.
Picha no. 5 Kaimu Mkuu wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka nchini Sierra Leonne na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) mara baada ya kumaliza ziara yao ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika.
Kaimu Mkuu wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwaeleza wageni kutoka nchini Sierra Leonne huduma zinazotolewa katika kliniki na wodi za watu maalumu na wagonjwa kutoka nje ya nchi wakati walipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika.
……………………….
Na Sophia Kingimali.
Timu ya wataalamu wa Wizara ya Afya kutoka Sierra Leone, wamefika nchini kujifunza namna ya kuanzisha matibabu ya moyo nchini kwao ambapo pia ililenga kukagua uwekezaji wa JKCI na kuingia makubaliano ya matibabu kwa kutibu wagonjwa kutoka nchini kwao kutibiwa hapa nchini.
Akizungumza leo Mei 3,2024 wakati akipokea ugeni huo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Piter Kisenge amesema ziara hiyo inalenga kuendeleza ushirikiano wa matibabu ya moyo kati ya Tanzania na Sierra Lione ikiwa ni dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ya kutangaza tiba utalii nchini, ikiendelea kuzaa matunda.
“Timu hii imefika hapa nchini, kujifunza uwekezaji wa matibabu ya moyo na usambazaji wa madawa na vifaa tiba kutoka kwa Bohari ya Dawa (MSD), ikiwa ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya Rais Dk. Samia,”amesema.
Amesema kuwa, timu hiyo ya wataalamu kutoka Sierra Lione imekiri kujifunza mambo mengi kutoka kwa JKCI, ambapo wataleta wagonjwa na wao kwenda kuanzisha taasisi yao kwa ushirikiano na taasisi hiyo.
Ameongeza kuwa, wataalamu hao wa Sierra Lione, wamejifunza utendaji kazi mkubwa na imara kutoka kwa watumishi wa JKCI, ikiwemo namna ya kuhudumia wagonjwa.
Ameeleza kuwa, hatua hiyo ya kupokea ugeni huo ni kubwa ambayo inatimiza malengo ya Rais Dk. Samia ya kukuza tiba utalii nchini.
Mkurugenzi Kisenge ameongeza kuwa, mbali na huduma za upasuaji wanazofanya Hospitalini hapo, wanaendelea kutoa huduma za upimaji wa moyo kupitia mpango wao wa Dk. Samia Tiba Mkoba ambao unasogeza huduma hizo karibu na wananchi huku wakizijengea uwezo Hospitali zingine za Kanda ikiwemo Benjamin Mkapa na zile za Chato na Geita.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Siera Lione, Sertie Kenneh, ambaye ni kiongozi wa msafara huo amesema, amefurahi kufika JKCI na kujifunza kazi kubwa ya matibabu ya moyo wanayoifanya kwa kuwa na uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba.
Ameipongeza serikali kwa uwekezaji mkubwa iliyofanya JKCI kwa kuwezesha matibabu ya magonjwa kwa wananchi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kuanzisha matibabu hayo.
“Tumejifunza vitu vingi namna ya utoaji huduma bora za matibabu kwa wagonjwa, ushirikiano uliopo baina ya watumishi wa taasisi ya JKCI kufanikisha lengo la huduma bora, hivyo nasisi tutaendelea kuimarisha ushirikiano,”amesema.
Amesema kwa ubora wa huduma walizoziona JKCI watapeleka wagonjwa wao kutibiwa hapo ili kupunguza gharama za kusafirisha wagonjwa kwenda ulaya.
Naye, Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa JKCI, Dk. Delila Kimambo, amesema mafanikio ya taasisi hiyo yanatokana na ushirikiano mkubwa walio nao watumishi wa Taasisi hiyo.
“Mafanikio haya yanayoonekana kwa ubora mkubwa katika kutoa matibabu sio ya jitihada za mtu mmoja, bali yanatokana na ushirikiano wa watumishi wote kuhakikisha tunafikia lengo lililokusudiwa,”amesema.
Amesema wataendelea kuimarisha ushirikiano na mataifa mbalimbali kuwavutia ili kuleta wagonjwa kutibiwa katika taasisi hiyo.