Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wakiwa katika matembezi ya Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliofanyika leo Mei 1, 2024 katika Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.
Mwana Jiolojia kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Denis Silas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliofanyika leo Mei 1, 2024 katika Uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.
Picha za matukio mbalimbali.
………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeungana na watumishi wote Duniani kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani, huku wakiwakumbusha watanzania kutumia mkaa mbadala kwa ajili ya kutunza mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 1, 2024 katika Maadhimisho ya Siku Wafanyakazi Duniani yaliofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Mwana Jiolojia kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Denis Silas, amesema kuwa wakati umefika kwa kutumia mkaa mbadala ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi.
Silas amesema kuwa STAMICO wameshiriki sherehe za Mei Mosi wakiwa sehemu ya wafanyakazi, huku akieleza kuwa wanaendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye kuleta tija kwa Taifa.
“Tuna mradi ya mkaa mbadala ambao ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya kutunza mazingira nchini, pia tuna wajimbaji wadogo wa madini ambao tunawasaidia kupata taarifa za jiolojia kwa ajili ya kuwasaidia kupata taarifa za kutekelezawa shughuli zao za uchimbaji wa madini” amesema.
Amefafanua kuwa pia wanafanya shughuli za uchorongaji wa mawe kupitia mitambo 14 ya kisasa katika kampuni za uchimbaji wa madini.
Hata hivyo ameeleza kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya uongozi wa STAMICO pamoja na wafanyakazi wake katika utekelezaji majukumu yao ya kila siku.