Serikali wilayani Njombe imekiri kukutana na wakati katika uetekelezaji wa kampuni ya chanjo ya saratani ya Mlango wa Kizazi kwa watoto wa kike wenye umri wa kuanzia miaka 9 hadi 14 ambapo inaelezwa baadhi ya wazazi na walezi walikuwa wakiwaficha watoto na wakidhani chanjo hiyo inaweza kuwasababishia madhara siku za mbeleni.
Ikumbukwe kampani ilipangwa kufanyika kimkakati kwa kupiti mashuleni ili kulifikia kundi kubwa kwa muda mfupi lakini pamoja na mpango ,bado matokeo yamekuwa hafifu kwasababu wazazi hawakuwaruhusu watoto wao kwenda shule ziku ambazo chanjo itafanyika.
Kufuatia changamoto hiyo ya watoto kufichwa ndani na kundi lingine la watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kushindwa kufikiwa ipasavyo kunamfanya mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa kutumia mkutano wa baraza la madiwani kuelimisha umma umuhimu wa chanjo hiyo kwa watoto wakike na majukumu ya viongozi jambo ambalo linatiliwa mkazo zaidi ya mganga mkuu halmashauri ya mji Njombe Jamal Juma ambae anasema vikwazo hivyo zimefanya kuchanja watoto 11,604 badala ya 13,109 na kuongeza siku
Baada ya serikali kubainisha changamoto zinazokwamisha kampeni hiyo na kisha kutoa agizo kwa viongozi wa serikali na siasa kuelimisha wananchi ndipo madiwani akiwemo Angela Mwangeni na Alatanga Nyagawa wakasema kinachowatesa ni utamaduni wa watu wa Njombe na uelezwa mdogo na kisha kueleza wanachokwenda kufanya ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha na kuwahimiza kuwaruhusu watoto wakike wapate chanjo hiyo muhimu kwa faida ya maisha yao na vizazi vijavyo.
Baadhi ya wakazi wa Njombe akiwemo Emmanuel Ngelime wanasema mwamko mdogo wa watu kupeleka watoto kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi imesababishwa na uelewa hafifu na utamaduni wa wakazi wa Njombe na kisha kutoa ushauri kwa serikali kuandaa makongamano na mikutano ya kueleimisha watu.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa ameagiza wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kuhama katika kipindi hiki cha mvua nyingi ili kujinusuru na mafuriko ambayo yamesababisha madhara makubwa maeneo mengi nchini ikiwa ni pamoja na kukatisha maisha ya watu.
Wakati mkuu wa wilaya akihimiza suala la chanjo ya saratani na tahadhali juu ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini ,Mwenyekiti wa halmashauri hiyo nae Erasto Mpete akawakumbusha watumishi na watendaji wa halmashauri hiyo kuendelea kubuni vyanzo vya mapato pamoja suala la maandalizi ya mwenge wa uhuru ambao uko mbioni kuingia mkoani Njombe.