Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania ( TPSF) ,Raphael Maganga akiwasilisha mada kwa wadau mbalimbali wa utalii katika kongamano hilo mkoani Arusha.
Wadau mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo mkoani Arusha
…………..
Happy Lazaro,Arusha .
Arusha .Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania ( TPSF) ,Raphael Maganga amesema kuwa baada ya kuzinduliwa kwa program ile ya Tanzania The Royal Tour, Sekta binafsi wameshuhudia ongezeko kubwa sana la watalii kutoka nje hadi kufikia takribani watalii 1.8 milioni mwaka 2023 sawa na ongezeko la 24.3% kutoka mwaka 2022, huku ongezeko pia la watalii wa ndani kufikia 1.9 milioni.
Ameyasema hayo mkoani Arusha leo wakati akizungumza katika kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya utalii lililowashirikisha wadau mbalimbali.
Maganga amesema kuwa,
Sekta ya utalii imeendelea kuongoza katika kuleta fedha za kigeni takribani USD 3.4 B mwaka 2023, katika kipindi ambacho nchini nyingi zilikumbwa na uhaba wa dola.
“Namba hizi kwa wengi wanaweza kudhani ni namba tu ambazo hazina maana kwao, lakini kwa wana Arusha lina maana kubwa sana. kwani, kutokana na ongezeko hili wanaweza kuwa mashuhuda kwani ajira za vijana wetu ziimeongezeka, miradi mipya ya kitalii inajengwa kama vile hoteli na camp sites, magari ya kitalii .”amesema Maganga.
Aidha amefafanua kuwa,sekta ya utalii imeendelea kuongoza katika kuleta fedha za kigeni takribani USD 3.4 B mwaka 2023, katika kipindi ambacho nchi nyingi zilikumbwa na uhaba wa dola.
Amesema kuwa,namba hizi kwa wengi wanaweza kudhani ni namba tu ambazo hazina maana kwao, lakini kwa wana Arusha lina maana kubwa sana, kwani, kutokana na ongezeko hili wanaweza kuwa mashuhuda kwani ajira za vijana wetu ziimeongezeka, miradi mipya ya kitalii inajengwa kama vile hoteli na camp sites, magari ya kitalii .
Aidha amefafanua kuwa, kila mmoja wetu anajua namna ambavyo mahoteli yalifungwa, wafanyakazi wakaachishwa kazi, familia nyingi hazikuwa na mwelekeo lakini mwaka 2022, na sote tulishuhudia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akifanya jambo ambalo wengi wetu hatujawahi kuona Mkuu wa nchi akifanya.
“kuvaa magwanda na kuingia field.. Master guide namba Moja.. kuitangaza Tanzania Dunia – Kupitia Tanzania The Royal Tour. Wengi, wetu hawakuweza kumuelewa na wengine wenye mioyo ya kutoamini, hawakuamini kwamba kutakuwa na siku Arusha itafurika watalii hata wakose nafasi (vitanda vya Kuwalaza wageni). “amesema Maganga.”amesema Maganga.
Ameongeza kuwa,kutokana na matokeo hayo makubwa yanahitajika kwa wingi mahitaji ya vyakula, mboga mboga, nyama yakiongezeka na kadhalikaa, hivyo hatuna budi kuipongeza serikali kwani huko tunakoelekea lazima tutegemee mafuriko, sio ya mvua bali ya watalii.
” Kutokana na ripoti ya UN Tourism 2020, ifikapo mwaka 2030. duniani kutakuwa na watalii bilioni 1.8. asilimia 88% ya watalii kote duniani watatokea bara la Asia. China peke yake ifikapo mwaka 2027, itakuwa na watalii takribani milioni 300,hii inamaanisha nini lazima kama Taifa tujiandae ipasavyo kuendelea kuwekeza katika sekta ya Utalii.”amesema .
Aliongeza kuwa , japo tumepiga hatua kubwa sana kufika watalii milioni 1.8, potential bado ni kubwa sana kwa Taifa letu kwa hali ya amani na Utulivu iliyopo nchini na vivutio tulivyonavyo nchini yaani mbuga, Wanyama, mito, bahari, utamaduni, na kadhalika , kufikia watalii 30 milioni ni jambo linalowezekana.
Maganga amesema kuwa,Fursa hizi lukuki zitawezekana iwapo haya 7 yatatiwa maanani kutoka sekta banafsi na sekta ya Umma, kwa Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi na Rafiki kwa uwekezaji na biashara kupita sera zinazotabirika na himilvu (Stable and predictable policy)
Ameongeza kuwa, Kutanua wigo wetu wa utalii – Kwa serikali kuendelea kufungua kanda za kusini, coast line kutoka Tanga hadi Mtwara, Kitulo National Park, Udzungwa Mountains, (mahale, Gombe, Katavi) (Jozani) .
Sekta Binafsi ya Tanzania kuendelea kuwekeza kwenye fursa zitokanazo na utalii kama vile hoteli, vyumba vya kulala (Air b n B), usafiri, chakula ,Uwekezaji katika utoaji huduma ( hospitality services) , Ujumuishaji wa Shughuli za Utalii katika Vivutio Vilivyopo Tanzania ili kuhakikisha fedha za kitalii zinaweza kuzunguka humu ndani na sio kulipiwa nje na kubaki nje.
Nyingine ni pamoja na utekelezaji wa mfumo wa ushuru na kodi za haki, na kuondoa kero katika ukusanyaji kodi pamoja na kwa wafanyabiashara,huku tukiendelea kuhakisha tunaendelea kulipa kodi stahiki ili kuiwezesha serikali .
Ambapo amezitaka sekta binafsi nchini kuchangamkia fursa hizi zitakazojitokeza na kuendelea kuwekeza katika sekta hii.