Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wakiwa katika matembezi ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliofanyika leo Mei 1, 2024 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Gari la TANESCO Mkoa wa Temeke likiwa limebeba mitambo ya umeme likipita katika Uwanja wa Uhuru katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Temeke wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa matembezi ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani
………
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke limeungana na watumishi wote Duniani kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani kwa kubeba mabango wakati wa matembezi ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo : Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga ya Hali Ngumu ya Maisha na Vyanzo mseto vya Nishati ndio jibu la umeme wa kutosha na wa uhakika.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo Mei 1, 2024 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaama ambapo watumishi wa Taasisi mbalimbali wameshiriki wakiwemo TANESCO Mkoa wa Temeke pamoja na viongozi ngazi ya Mkoa huku Mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salamm Mhe. Albert Chalamila.