Na Sophia Kingimali.
Mkuu wa Chuo cha Furahika David Msuya ameipongeza Jumuiya ya Wazazi CCM nchini kwa jitihada zao za kupeleka watoto kwenye mradi wa elimu bure unaoendeshwa chuoni hapo huku akitoa rai kwa wazazi kuhakikisha wanapeleka watoto wao kupata elimu ya ujuzi ili waweza kujiajili na kuajiliwa.
Wito huo ameutoa leo Mei 1,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kupokea wanafunzi wa kozi ndefu ambao wapo nje ya mradi ambao watasoma chuoni hapo kozi mbalimbali kwa gharama nafuu.
Amesema chuo hiko si kwa ajili ya wanafunzi waliofeli tu bali ni kwaajili ya wanafunzi wote wenye nia ya kutimiza ndoto zao kupitia taaluma mbalimbali.
“Mimi nataka niwaambie Furahika si kwaajili ya waliofeli tu hapa tunapokea wanafunzi wote aliepata hata alama D moja atapata elimu na ambae hana hata D pia atapata elimu kupita mradi wa elimu bure kwa tunapokea hata wa darasa la saba kwenye fani kama ya umeme,Fundi bomba tunajua tunamfundishaje na atafanya myihani kama kawaida”,Amesema Msuya.
Amesema kutokana na kumuunga mkono ya Dkt Samia Suluhu Hassan kozi ambazo zinatolewa za muda mrefu ambazo hazipo kwenye mpango wa elimu bure zinatolewa na bei rahisi tofauti na vyuo vingine kwani lengo lao ni kuhakikisha hakuna mtoto anaebaki nyumbani kwa kushindwa kulipa ada ili kupunguza wimbi kubwa la watoto mitaani ambao wanajiingiza kwenye makundi yasiyofaa.
Sambamba na hayo Msuya amempongeza waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi Profesa Adolf Mkenda kwa jitahada na ushauri wake katika sekta ya elimu nchini.
Pia ametoa Rai kwa Jumiya ya wazazi CCM kuhakikisha wanaendelea kuhamasisha vijana katika mikoa mbalimbali kuja kusoma chuoni hapo kwani wanahuduma ya ‘Hostel’ ambayo inapatikana kwa gharama ndogo lakini pia mazingira ni mazuri kwa ajili ya kujifunzia.