Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiendesha kikao na wadau wa uwekezaji wa biashara ya kaboni kutoka Kampuni ya Shiftling na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kikao na kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 30 Aprili, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa uwekezaji wa biashara ya kaboni kutoka Kampuni ya Shiftling na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kikao na kilichofanyika jijini Dodoma leo tarehe 30 Aprili, 2024.
…………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya kikao na wadau wa uwekezaji wa biashara ya kaboni jijini Dodoma leo tarehe 30 Aprili, 2024.
Wadau hao ni kutoka Kampuni ya Shiftling ambao wamewasilisha wasilisho la namna watakavyotekeleza mradi huo katika teknolojia ya ukusanyaji wa taarifa za kaboni hapa nchini.
Akizungumza na wadau hao, Waziri Dkt. Jafo amesema huo ni mpango mzuri ambao utasaidia kukusanya taarifa za hewa ya ukaa inayopatikana katika maeneo mbalimbali nchini.
Hatua hiyo ni kuunga mkono biashara ya kaboni ambayo inafanyika katika kuihifadhi mazingira kwa kupanda miti kwa wingi.
Amewataka wadau hao kuanda andiko la mradi huo na kuuwasilisha kwa timu ya wataalamu wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ajili ya kupitiwa na kujadili hatimaye kuwasilishwa kwa viongozi kwa hatua zaidi.
Ujumbe wa wadau hao umeundwa na viongozi kutoka China na Kenya. Kwa upande wa Ofisi ya Makamu wa Rais imewakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Bi. Kemilembe Mutasa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bw. Dustan Shimbo.