Timu za Shirika la umeme Tanzania (TANESCO SC) zimefanikiwa kutwaa makombe matano kwenye mashindano ya michezo ya Mei Mosi 2024 yanayofanyikia mkoani Arusha.
Fainali za mashindano hayo zimefunguliwa tarehe 29/04/2024 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ambapo mchezo wa Mpira wa miguu ulichezwa kati ya timu ya Tanesco na timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani huku mchezo huo ukiisha kwa sare ya bao moja kwa moja kwa kila timu ambapo matokeo hayo yalipelekea timu hizo kuenda hatua ya matuta na timu ya Tanesco iliibuka na ushindi wa penati tatu (3) chini ya nahodha Zuberi Sebiga huku timu ya mambo ya ndani ikiambulia penati moja (1) kati ya penati nne (4) zilizopigwa na timu zote mbili.
Pamoja na kombe hilo kubwa, timu za Tanesco zimefanikiwa kutwaaa makombe mengine ambayo ni; Mshindi wa pili Volleyball (ke), mshindi wa pili mchezo wa draft (me), Mshindi wa tatu Volleyball (me), na mshindi wa tatu karata (me). Huku michezo mingine kama Netball na visale timu hizi zikiishia hatua ya robo fainali.
Kombe hilo la mshindi wa kwanza wa mpira wa miguu litakabidhiwa kwa timu ya TANESCO na raisi wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ndio atakaye kuwa mgeni rasmi siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yatakayofanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Mei 1, 2024 mkoani Arusha.