Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Tanzania Benoite Araman akabidhi mitungi ya gesi ya kilo 15 na jiko lake kwa mwandishi Halima Mlacha wa gazeti la Habari leo katika hafla iliyofanyika kwenye ‘Depot’ ya gesi ya kampuni hiyo iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Tanzania Benoite Araman akabidhi mitungi ya gesi ya kilo 15 na jiko lake kwa mwandishi Suleiman Mpochi wa gazeti la Guardian katika hafla iliyofanyika kwenye ‘Depot’ ya gesi ya kampuni hiyo iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Tanzania Benoite Araman akimsaidia kubeba mtuingi wa gesi Bw. Suleiman Mpochi mara baada ya kukabidhiwa jiko lake na mtungi wa gesi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Tanzania Benoite Araman akabidhi mitungi ya gesi ya kilo 15 na jiko lake kwa mwandishi Hellen Mwango wa gazeti la Uelekeo katika hafla iliyofanyika kwenye ‘Depot’ ya gesi ya kampuni hiyo iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Meneja Miradi wa nishati safi ya kupikia kutoka Oryx Peter Ndomba akifafanua jambo katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Tanzania Benoite Araman akisoma taarifa yake kabla ya kugawa mitungi hiyo na majiko ya gesi kwa waandishi wa habari na wahariri.
Picha ya pamoja.
………………………….
Na Sophia Kingimali.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Tanzania Benoite Araman ametoa rai kwa waandishi na wahariri kuendelea kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa umma ili kuhakikisha lengo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati hiyo linakamilika ili kulinda afya zao na mazingira.
Wito huo ameutoa leo April 30,2024 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi ya kilo 15 na jiko lake kwa waandishi na wahariri iliyofanyika katika ‘Depot’ ya gasi iliyopo Kigamboni jijini hapo.
Amesema Oryx wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo adhma hiyo ya Rais kwani mpaka sasa wameshagawa mitungi ya gesi 33000 kwenye maeneo mbalimbali yenye thamani ya shilingi bilioni 1.5.
“Tunaahidi kama ilivyo siku zote tutaendelea na kampeni hii kadri ya uwezo wetu ili kuhakikisha tunaunga mkono kwa vitendo jitahada za Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha anamsaidia mwananchi hasa mwanamke kumtua kuni kichwani na kulinda afya yake na mazingira”,Amesema Benoite.
Akizitaja faida za kutumia gesi ya Oryx amesema matumizi ya gesi kwenye taasisi yanasaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji na kupunguza muda wa taasisi hiyo kutafuta nishati mbadala kama kuni na mkaa.
Aidha amesema kupikia kwa gesi hiyo kunalinda afya na mazingira na kutokomeza ukatiji lakini pia kunamsaidia kulinda afya mwanamke ambao wanaathirika kwa moshi unaotokana na mkaa na kuni.
“Kutumia gesi hii kunalinda mazingira kwa kutunza misitu kwani misitu hiyo ni muhimu kwa viumbe hai,kuhifadhi udongo,kusaidia mzunguko wa maji lakini pia kulinda ekolojia na rasilimali za asili”,Amesema na kuongeza kuwa
“Wanawake wanaathirika kwa kutumia kuni na mkaa kwani moshi unachembechembe za sumu ambazo husababisha magonjwa kama Pneumonia,Cancer ya Mapafu na matatizo ya upumuaji”,amesema.
Akitaja sababu nyingine ya kutumia gesi hiyo pia ni kupunguza ukatili unaowapata wanawake na watoto pindi wanapoenda kutafuta kuni misitu pia kuepuka kujeruhiwa na wanyama wakali hivyo kwa kufanya hivyo itawaokolea muda na kuweza kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.
Kwa upande wake Meneja Miradi wa nishati safi ya kupikia kutoka Oryx Peter Ndomba amesema wameendelea kutoa hamasa na elimu kwa wananchi kutunza fedha kidogo kidogo ili pindi gesi inapoisha waweze kujaza lakini pia wameshaongea na benki ya TPB kuweza kusaidia wananchi kupeleka pesa kidogo kidogo kwa ajili ya kununulia gesi pindi inapoisha.
Aidha amesema 2021 walikua na mradi wa kijiji hadi kijiji ili kuhakikisha wanakuwa na wasambazi ambapo baada ya hapo waliingia zoezi la nyumba hadi nyumba ili kuhakikisha nishati hiyo inaweza kumfikia kila mwananchi na kuachana na kutumia nishati chafu.
“Tanzania inanyumba takribani milioni 14 na kati hiyo ni milion mbili tu ndio zinatumia na sisi lengo letu kuhakikisha angalau nyumba milioni 8 zinatumia nishati hii ya Oryx”,Amesema Ndomba.
Ameongeza kuwa mitungi yao ya gesi ni salama na imewekwa alama zote za usalama pindi mtumiaji anapotumia anaweza kuzitumia taratibu hizo ili kuendelea kuwa salama lakini pia wanaendelea kutoa elimu mara kwa mara ya namna bora na salama ya kutumia mitungi hiyo.
Amesema wamekuwa wakigawa mitungi ya gesi na majiko kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya baba na mama lishe watumishi wa sekta ya afya na wajasiliamali