Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo (Aprili 30, 2024) ameshiriki katika semina ya wabunge, Jijini Dodoma ambapo miongoni mwa yaliyojiri ni upatikanaji wa umeme vijijini, matumizi ya gesi asilia katika magari na uimarishaji wa umeme kupitia gridi ya Taifa.
Wabunge pia wamezungumzia umuhimu wa matumizi ya Nishati Safi ya kupikia sambamba na kupokea majibu ya maswali yaliyoibuliwa wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyohitimishwa tarehe 19 Aprili, 2024 Jijini Dodoma.