Na Farida Mangube
Mabalozi wa nchi za umoja wa Ulaya wamakitembelea Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA, Kampasi ya Edward Moringe, ili kujionea miradi mbalimbali inayoendelea Chuoni hapo kwa ufadhili wa nchi wanachama wa Jumuia hiyo.
Mabalozi hao wakiongozwa na Balozi wa Jumuia ya Ulaya na Jumuia ya Afrika Mashariki Mhe.Christine Grau, wamepokewa Chuoni hapo na Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Rafael Chibunda na kupata fursa kufanya mazungumzo na menejimenti ya SUA na kusikiliza Mawasilisho mbalimbali kutoka kwa Wahadhiri wa SUA shughuli iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo hicho.
Katika ziara hiyo Mabalozi hao pia wametembelea Kituo cha Hewa Ukaa kilichopo SUA, na kupata maelezo ya kina kuhusu kituo hicho kinavyofanya kazi kutoka kwa msimamizi wa Kituo hicho Prof.Eliakim Zahabu na kueleza namna, kituo kinavyopokea maandiko mbalimbali kutoka kwa taasisi na watu binafsi zikieleza namna zinavyoweza kubuni shughuli rafiki kwa mazingira ili kupunguza athari za Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.
Katika Kituo cha Hewa Ukaa Mabalozi wamepata nafasi ya kuuliza maswali na wamefurahishwa na kazi zinazofanyika kituoni hapo na pia wametaka kujua Sera na Mipango ya kuthibiti hewa ukaa na kuifanya kuwa fursa kwa wananchi ambapo msisitizo umewekwa kwa kupanda miti kwa wingi ambayo hufyonza hewa ukaa inayosabibishwa kwa kiasi kikubwa na maendeleo ya viwanda ulimwenguni.
Kwa upande wa Kituo cha kufundishia Panya mabalozi pia wamepata maelezo kutoka kwa Afisa habari wa kituo hicho Madam Lily Shallom na kupata maelezo ya kina kuhusu APOPO na fursa ya kujionea namna ya panya wanavyotumika kugundua vitu vilivyofichwa ardhini.
Kwa upande wake naibu Makamu Mkuu wa Chuo Fedha, Mipango na Utawala Prof . Amandus Muhairwa amesema Mabalozi hao kutoka Jumuia ya Ulaya, ujio wao ni kutokana na uwepo wa Miradi ambayo inayofadhiliwa na Nchi wanazotoka Mabalozi hao lakini pia wamekuja kuzungumza na Vijana ambao ndio wanufaika wa miradi hiyo.
Prof. Muhairwa amesema,Chuo kitaendeleza mahusiano mema na Jumuia hiyo, kutokana na SUA, kutokana na Chuo kuendelea vizuri, miradi iliyopo chuoni hapo na hivyo kuendeleza mahusiano mema.
‘’Kwa upande wa Chuo hii ni nafasi mojawapo ya wao kujionea ambacho kinaendelea,na tunauhakika kwamba kile kilichofanyika kinaridhisha kisi cha kwamba tunaweza tukaendelea na mahusiano,na hawa mabalozi kama wafadhili wetu wa miradi inayoendelea hapa Chuoni,amesema Prof. Muhairwa.
Kiongozi wa Mabalozi Mhe.Christine Grau ambae ni Balozi wa Jumuia ya Ulaya na Jumuia ya Afrika Mashariki,katika safari yao wapo waheshimiwa mabalozi kutoka nchi za Ubelgiji,Finland, Ufaransa, Italia, Uholanzi, Denmark, Sweden, Jamhuri ya Ireland na kusema wamefurahishwa na maendeleo ya miradi inayoendelea SUA.
Amewataka vijana wa Kitanzania ambao wamepata fursa ya kufika elimu ya juu kutumia muda wao vizuri ili waweze kufaulu vizuri masomo na waweze kututa changamoto za jamii wanazotoka ikiwepo suala la Athari ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.