Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange (Mb) amewaelekeza wataalamu na wasimamizi wa Mageti katika Halmashauri kuacha kutoza Ushuru wakulima wanaosafirisha Mazao chini ya Tani moja ndani ya Halmashauri husika na kufuata utaratibu wa kiwango cha kutozo kisichozidi asilimia tatu ya mazao yaliochini ya Tani moja kwenda nje Halmashauri.
Dkt. Dugange amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu, wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Jimbo la kilombero Mhe. Abubakar Damian Asenga (Mb) aliyehoji je Kwanini Wananchi wa Wilaya ya Kilombero wanatozwa Ushuru wa Mazao chini ya Tani moja katika Geti la Idete, Kivukoni na Kidatu kinyume na maelekezo ya Serikali.
´Ni kosa na niuvunjifu wa sheria kwa watalaamu au wasimamizi kutoza ushuru kwa wakulima wa ndani ya Halmashauri wanaosafirisha Mazao chini ya Tani moja ndani ya Halmashauri na tutachukua hatua za kinidhamu kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo” Dkt. Dugange
Aidha Dkt. Dugange amezielekeza Halmashauri zote nchini kutowatoza Ushuru Wakulima wa kawaida wa ndani ya Halmashauri wanaotoa Mazoa yao shambani kupeleka nyumbani, amesema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge la Jimbo la Bukene, Mhe. Suleimani Zedi (Mb) aliyetaka kujua, Je Serikali ipo tayari kutoa katazo kwa wataalamu watoza ushuru waache kuwatoza ushuru wakulima wa kawaida ambao sio wafanyabiashara?
“sheria ya ushuru wa mazao inaeleza wazi kwamba nimarufuku na haitakiwi kutoza ushuru kwa wakulima wakawaida ambao wanatoa mazao yao shambani na kurudisha nyumbani ndani ya Halmashauri” Dkt. Dugange.