Walimu ,wanafunzi na wazazi wa shule ya sekondari Mount Kipengere Iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Njombe Wameiomba serikali kukamilisha ujenzi wa jengo la Utawala pamoja na kutafuta muarobaini wa changamoto ya ukosefu wa huduma za afya katika eneo hilo la shule linakusanya mamia ya wafunzi.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kipengere wakiongozwa na diwani wa kata hiyo Mussa Sanga na Neema Nziku mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Kipengere wameeleza ukubwa wa tatizo la matibabu na adha ya kukosa jengo la utawala inavyoathiri taaluma shuleni hapo na kisha kumuomba mkuu wa mkoa kuwasaidia kupata utatuzi.
Mh Sanga amesema wananchi walitambua umhimu wa kukamilisha ujenzi huo lakini licha ya kupambana kuchangishana lakini wameshindwa kumaliza hivyo wanaomba kushikwa mkono
Mara baada ya kupokea changamoto hiyo ndipo mwakilishi wa mkurugenzi wa halmashauri ya Wanging’ombe ambaye ni afisa mipango Nicefrus Mgaya akasema tayari serikali imetenga fedha katika bajeti ya kukamilika ujenzi huo mwaka ujao huku pia akiahidi kuendelea kusimamia miundombinu hiyo ilikuwa na manufaa kwa wananchi
Ahadi iliyotolewa na halmashauri kuhusu jengo la utawala na huduma za afya zinamuibua mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka katika mkutano kuwataka wanafunzi kutunza miundombinu ya shule hiyo iliyogharimu zaidi ya mil 800 na kuwakumbusha majukumu yao wanafunzi waliyo madarasa ya mitihani.
“Nafanya ziara kwenye maeneo muhimu ikiwemo taasisi za elimu ili kuhamasisha wanafunzi kutekeleza jukumu lao la kusoma na kufanya vyema katika mitihani yao”alisema RC Mtaka.