Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Prof.Lazaro Busagala akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo Aprili 29,2024 jijini Dar es salaam katika kikao kazi cha Msajili wa Hazina, Wahariri wa habari na taasisi hiyo Aprili 29, 2024.
Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Prof.Lazaro Busagala akifafanua jambo akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo Aprili 29,2024 jijini Dar es salaam katika kikao kazi cha Msajili wa Hazina, Wahariri wa habari na taasisi hiyo Aprili 29, 2024.
Sabato Kosuri Afisa Habari Mwandamizi Ofisi ya Msajili wa Hazina akichangia hoja wakati akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo Aprili 29,2024 jijini Dar es salaam katika kikao kazi cha Msajili wa Hazina, Wahariri wa habari na taasisi hiyo Aprili 29, 2024.
……………………….
Tume ya Nguvu za Atomi nchini (TAEC) inajivunia mafanikio makubwa waliyoyapata katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani wameweza kupiga hatua kubwa ya kimaendelea ambapo wameweza kujenga majengo 6 ya maabara na ofisi katika kanda tano yenye thamani ya bilioni 28.11
Akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari leo Aprili 29,2024 jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa TAEC Prof. Lazaro Busagala amesema katika kipindi kifupi cha Rais Dkt Samia wameweza kusogeza huduma zaidi kwa wananchi na kuwahudumia kwa kutumia Tehama.
“Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuwasogezea wananchi huduma kwa kujenga miundombinu mbalimbali ambayo inaipa uwezo TAEC wa kutoa huduma kwa wananchi kwa tija na kwa ukaribu”,Amesema.
Amesema uwepo wa maabara hizo za teknolojia ni muhimu kwa wananchi kwani zinasaidia kuokoa muda na pesa kama ilivyokuwa awali ambapo sampuli zililazimika kusafirishwa kupelekwa maabara.
Ameongeza kuwa TAEC imekasimiwa kukusanya maduhuli ya serikali hivyo wanajivunia mafanikio kwani makusanyo ya Maduhuli hayo imeongezeka kutoka Bilioni 8 mpaka Billion 10.9 ambapo hiyo imechagizwa na serikali kutengeneza mifumo mizuri ya Tehama kwani imesogeza huduma kwa wananchi.
Sambamba na hayo amesema TAEC imepunguza muda wa utoaji wa cheti cha uchunguzi wa mionzi kutoka siju 7 awali mpaka masaa matatu ambapo pia muombaji anaweza kutumia mfumo kuomba popote alipo na akapewa cheti
Aidha ameongeza kuwa TAEC wameondoa tozo kwa huduma zote wanazozitoa ambapo serikali inagharamia gharama zote za upimaji sampuli na tozo hiyo inawahusu hasa wafanyabiashara wadogo lakini wafanyabiashara wakubwa wanaosafirisha bidhaa nje ya nchi wao imepunguzwa kwa asilimia 50.
Amesema Serikali ya awamu ya sita pia imesaidia kuongeza matumizi ya Tehama kwani sasa mifumo inaweza kusomana na mfanyabiashara anaweza kufanya kila kitu popote anapokuwa hali inayosaidia kuokoa muda na gharama.
Akizungumzia kuhusu rasilimali watu amesema serikali imeweka mpango wa kusomesha vijana watano nje ya nchi kila mwaka ili kujifunza teknoliojia mpya ambayo bado nchi haijaifikia lakini pia serikali inaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi ambapo mpaka sasa watumisi 26 wameshalipiwa na wanaendelea na masomo katika ngazi mbalimbali.