Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Dkt.Selemeni Jafo akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya
gesi 1500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha
wakiwemo wajasiriamali tarehe 27 Aprili,2024 jijini Arusha Mikutano
Arusha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Dkt.Selemeni Jafo na viongozi mbalimbali wakimkabidhi mtungi wa gesi
ya kupikia wa Oryx mmoja wa mama lishe wa Mkoa wa Arusha wakati wa
hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1,500 yakiwa na majiko yake kwa
wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali tarehe 27 Aprili, 2024.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Dkt.Selemeni Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya gesi ya Oryx Bw. Benoite Araman wakati wa hafla ya
kukabidhi mitungi ya gesi 1,500 yakiwa na majiko yake kwa wananchi wa
Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali tarehe 27 Aprili, 2024.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Dkt.Selemeni Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali
wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1,500 yakiwa na majiko
yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha wakiwemo wajasiriamali tarehe 27
Aprili, 2024.
………………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Dkt. Selemeni Jafo amesema takwimu zinaonesha watu milioni nne
barani Afrika wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na matumzii ya
nishati chafu ikiwemo ya kuni na mkaa.
Hivyo, amesema ajenda ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya
kuanzisha kampeni ya kuhamasisha nishati safi Afrika inapaswa kuungwa
mkono na watu wote.
Amesema kuwa matumizi ya kuni na mkaa nchini yanasababisha hekta
takriban 46,242 kupotea kila mwaka kwa kukatwa kwa ajili ya kupata
kuni na mkaa.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 1,500 yakiwa
na majiko yake kwa wananchi wa Jiji la Arusha tarehe 27 Aprili, 2024
wakiwemo wajasiriamali, Dk. Jafo amesema hatua hiyo inaunga mkono
juhudi za Rais Samia katika kampeni ya kuhamasisha nishati safi.
“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amekuwa na dhamira njema na ndio
maana amekuja na kampeni ya nishati safi ya kupikia.Haya ni mapenzi
yake na kwasababu tunafahamu nishati chafu inamadhara makubwa
katika mazingira.
“Kwanza watu wanalazimika kutegemea kuni na mkaa kwa hiyo kuna
uharibifu wa mazingira. Takwimu zinaonesha kila mwaka hekta 4,6242
zinapotea kwasababu ya kuni na mkaa,”amesema Dkt. Jafo.
Pia amesema takwimu zinaonesha kuwa wakinamama na wasichana kwa
asilimia kubwa wanatumia wastani wa saa 20 kwa wiki kwa ajili ya
kutafuta kuni na mkaa au wakati mwingine ni kinyesi cha wanyama.
“Leo hii ukiona nchi imejipanga katika nishati safi ya kupia ni jambo la
msingi lenye kutia matumani.Watafiti wanatuambia kitendo cha kutumia
nishati safi ya kupikia kwa akina mama wajazito kunasaidia kurekebisha
presha ya mama mjazito,”amesema.
Ameongeza pia nishati safi inasaidia mama mjazito kupata mtoto
mwenye uzito unaokubalika anapozaliwa , hivyo kuna faida nyingi
kutumia nishati safi ya kupikia.
“Nina fahamu mpaka leo hii Oryx wameshatoa mitungi ya gesi 32,000
kwa ajili ya jamii na wameshatumia Sh.bilioni 2.7 lakini bado
wameendelea kuendelea na kampeni hiyo kwa kutoa mitungi kwa jamii.
Ameongeza kuwa Oryx wamekuwa mfano mzuri kuifikia jamii huku
akifafanua tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwa taasisi zinazoanzia
watu 100 kufunga mfumo wa kutumia nishati safi ya kupikia na tayari
taasisia na mashirika ya umma yameanza kutumia nishati hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema
katika kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia kuhamasisha nishati safi
ya kupikia wameona ni vema kuendelea kuyagusa makundi mbalimbali
katika jimbo hilo.
Amesema kuwa kabla ya kugawa mitungi hiyo 1,500 ya Oryx kwa wana
Arusha Mjini, tayari ameshagawa pia mitungi 1400 kwa wajasiriamali
huku akisisitiza wataendelea na kuyafikia makundi yote yakiwemo ya
watoto wanaolelewa vituo vya ya watoto yatima.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya gesi ya Oryx Bw.
Benoite Araman amesema madhara yanayotokana na kutumia kuni na
mkaa ani makubwa na kuwa wananchi 33,000 wanapoteza maisha kila
mwaka kwa kuvuta moshi na chembe chembe zinazotokana na mkaa na
kuni, hivyo kupikia gesi itatatua jambo hili.
Amesema kupika kwa kutumia gesi huchochea kutokukatwa kwa miti
kwa ajili ya kuni na mkaa hivyo, husaidia kulinda mazingira na wakati
huo huwafanya wanawake wasitumie muda mwingi kutafuta kuni na
msituni hatua itakayosaidia maandalizi ya chakula kwa wakati.
"Oryx Gas Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutekeleza
maono ya Rais kuhusu upatikanaji wa nishati. Namshukuru Mbunge wa
Arusha Mjini Gambo na Serikali ya Tanzania kwa kutuunga mkono katika
mipango yetu ya nishati safi kwa kuhakikisha matumizi ya gesi ya Oryx
hapa Arusha na Tanzania kwa ujumla,". Amesema Bw. Araman
Wakitoa shukrani zao Wajasiriamali Bi. Asha Mtumwa na Bw. Karim
Abdallah wakieleza kuwa hatua hiyo ya kukabidhiwa mitungi ya gesi
inakwenda kuwaondolea adha waliyokuwa wakiipata kwa muda mrefu.
Wamesisitiza kuwa inaenda kuondoa athari ambazo zimekuwa
zikijitokeza kwa matumizi ya kuni na mkaa ambapo inaathari kuanziakwenye afya pamoja na mazingira sanjari na kuokoa gharama za mkaa
ambazo ni kubwa zaidi.